24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Wamarekani wapiga kura kuamua mwelekeo wa utawala wa Trump

CALIFORNIA, MAREKANIWAMAREKANI jana walipiga kura katika uchaguzi wa katikati ya muhula, ambao utasaidia kutoa mwelekeo wa hatma ya miaka miwili iliyosalia ya muhula wa kwanza ya uongozi wa Rais Donald Trump.

Viti 435 katika Baraza la Wawakilishi pamoja na viti 35 vya Seneti na 39 vya ugavana vinagombewa kwenye uchaguzi huo.

Chama cha Rais Trump cha Republican kwa sasa kina viti vingi katika Seneti na Baraza la Wawakilishi, lakini iwapo kitashindwa kuvidhibiti katika uchaguzi huu, huenda hali hiyo ikachangia mkwamo wa kisiasa wa sera za Rais Trump.

Kwa mujibu wa kura za maoni, Chama cha Democrat kina nafasi nzuri ya kudhibiti Baraza la Wawakilishi, huku wana-Republican wakitabiriwa kuendelea kudhibiti Seneti.

Uchaguzi huo ni wa kwanza  tangu Urusi ilipoilenga mifumo ya uchaguzi nchini hapa mwaka 2016 wakati wa uchaguzi wa rais.

Maofisa wote wa uchaguzi wamesema wameweka juhudi zote kuhakikisha mifumo hiyo iko salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles