27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wamarekani wanasubiri kujua nani atashinda urais

WASHTON, MAREKANI

Huenda Wamarekani wakakesha Jumatano ya leo kabla ya kujua nani atakuwa rais wao mpya kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo kwenye uchaguzi huu uliofanyika wakati taifa hili limegawika sana kwa mara ya kwanza tangu vita vya Vietnam miaka 1970.

Kura zinahesabiwa katika majimbo yote hivi sasa na katika majimbo ya mashariki inaonekana wagombea hao wawili wanapata ushindi katika ngome zao za kawaida wakati ushindani uko katika majimbo mengi na imekuwa vigumu kutabiri nani atapata ushindi.

Marekani ushindi unategemea zaidi katika majimbo kwani kila mmoja anagombania wajumbe wa majimbo hayo kuweza kushinda uchaguzi. Kuweza kupata ushindi mgombea kiti cha rais anahitaji kupata kura 270 za wajumbe wa majimbo.

Mapema leo hali ilikuwa inaonyesha kuwa, Biden anaongoza akiwa na kura 205 za wajumbe wa majimbo na Trump ana 100.

Kwa upande wa Baraza la Senate kila kipindi cha uchaguzi theluthi moja tu ya viti vinashindaniwa hivyo kuna viti 35 vinagombania na wademokrat wanahitaji viti vitatu au vinne zaidi kuchukua udhibiti kutoka wa Republikan.

Mbali na mashindano hayo ya kiti cha rais kuna mashindano ya wajumbe wa Bunge Kuu la Marekani ambao wabunge wote 435 wa baraza la wawakilishi au baraza kuu la bunge wanagombea kiti, lakini wachambuzi wanasema Wademokrats wataendelea kulidhibiti baraza hilo wakiongeza viti vitano.

Katika uchaguzi huu kuna viti saba vinavyoshikiliwa na Warepublican vyenye ushindani mkubwa na utafiti unaonyesha huenda Wademokrat wakanyakua baadhi ya viti hivyo hadi sasa wamenyakua kiti kimoja zaidi.

Uchaguzi huu unachukuliwa wa kihistoria kutokana na idadi ya watu walioshiriki ambapo watu milioni 100 walipiga kura mapema au kwa njia ya posta na zaidi ya milioni 150 wamepiga hiyo jana

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles