Waliovamiwa na tembo kisha kula chakula cha akiba, wapewa msaada wa mahindi

  0
  641
  Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu Dkt. Joseph Chilongani akikabidhi msaada wa mahindi kwa wananchi ambao walivamiwa na tembo kutoka pori la akiba la Maswa, ambapo mahindi hayo yametolewa Mamlaka ya ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA)

  Derick Milton, Meatu

  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa msaada wa mahindi gunia mbili kwa kila familia zinazopakana na pori la akiba la Maswa katika kata za Mwasengela na Tindabuliga  Wilayani Meatu Mkaani Simiy ambazo hivi karibuni zilivamiwa na tembo.

  Tembo hao ambao wanatoka kwa pori hilo walivamia jumla ya kaya 39 kutoka katika kata hizo na kuaribu nyumba kisha kila chakula chote ambacho kilikuwa kimehifadhiwa yakiwemo mahindi, mtama, mihogo, viazi pamoja na unga.

  Akikabidhi msaada huo leo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Joseph Chilongani, Meneja wa Pori hilo Lusato Masinde amesema kuwa, msaada huo unatokana na ahadi ya Kamishna Mkuu wa Uhifadhi toka Mamlaka hiyo nchini Dkt.James Wakibara aliyoitoa Septemba 9, 2019 wakati alipotembelea familia hizo.

  “ Kamishna baada ya kuoga uharibu ule kama binadamu aliona ni vyema mamlaka ukatoa msaada huu kama pole lakini pia kuwasaidia wananchi ambao mazao yao yote yaliliwa, leo tutawakabishi gunia mbili kila kaya ambazo ziko 39 zilizopatwa na janga hili,” alisema Msinde.

  Aidha Meneja huyo aliendelea kuwasisitiza wananchi wanaopakana na hifadhi hiyo, kuendelea kuweka tahadhari juu ya wanyama hao ambao alieleza kutokana na uhifadhi wamekuwa wengi na wanavamia maeneo ya wananchi kila mara.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya huyo aliushukuru uongozi wa TAWA kwa msaada huo ambao utawasaidia wananchi ambao walibaki bila chakula, huku akiwasisitiza wananchi kutumia vikundi vya vijana ambavyo vilipewa mafunzo ya jinsi gani ya kuwazuia wanyama hao ili wasiendelee kuleta madhara kwao.

  LEAVE A REPLY

  Please enter your comment!
  Please enter your name here