28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

WALIOSHTAKIWA KWA RUSHWA KENYA KUKAA RUMANDE WIKI MOJA

NAIROBI, KENYA


WATUHUMIWA 24 walioshtakiwa kuhusu kashfa ya ufujaji wa fedha katika Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa wiki moja.

Jaji ameamuru wazuiliwe hadi Jumatatu wiki ijayo uamuzi wa kuachiliwa kwa dhamana utakapotolewa.

Miongoni mwa walioshtakiwa juzi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia, Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa NYS, Richard Ndubai.

Walikamatwa na wengine wakajisalimisha kwa polisi Jumatatu wiki hii na kisha kufikishwa kortini Milimani, Nairobi jana.

Kikao cha kusikilizwa kwa kesi dhidi yao kiliendelea hadi usiku wa manane.

Upande wa mashtaka ulipinga washukiwa kupewa dhamana, ukisema wanaweza kutoroka au kukosa kurejea mahakamani wakati wa kusikizwa kwa kesi dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,491FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles