23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waliopoteza vitambulisho watapiga kura – NEC

Lubuva+PHOTONA JONAS MUSHI, DAR ES SAALAM

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura wataweza kupiga kura endapo watakuwa na taarifa ya polisi  na majina yao kuwamo katika  daftari la mpiga kura.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Kamishna wa NEC, Mary Stelalongwe alipotoa ufafanuzi kuhusu  watu wanaozunguka mitaani kuandika namba za vitambulisho vya wapiga kura.

Alionya kuwa kufanya hivyo ni kosa ingawa alisema  NEC haina  taarifa rasmi ya matukio hayo.

Wakati huohuo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema tume imepeleka taa katika vituo vyote vya kupigia kura   kuepuka kura kuhamishwa na   kuhesabiwa sehemu nyingine.

“Tunasema kura zitahesabiwa katika kituo husika lakini inapotokea hiyo sehemu haina taa inabidi kura hizo zihamishiwe katika kituo chenye taa ambako zitasindikizwa na mawakala na zitatenganishwa na za kituo hicho,” alisema Lubuva.

Alisema ili kuepuka hali hiyo Tume  imesambaza taa katika vituo vyote vya kupigia kura ambavyo ni 72,000 nchi nzima.

Akizungumzia   mchango wa vyombo vya habari katika uchaguzi huu, aliviomba viisaidie tume kutoa taarifa sahihi   uchaguzi uwe wa amani.

“Vyombo vya habari vikiwa mstari wa mbele na kufanya kazi yake kwa umakini bila kupotosha vitaisaidia Tume iendeshe uchaguzi katika hali ya amani na utulivu,” alisema Lubuva.

Alisema  vyombo vya habari havitaruhusiwa kutangaza mshindi wa uchaguzi kabla ya kutangazwa na mamlaka husika lakini wanaruhusiwa kuripoti matokeo ya vituoni kama yalivyo.

Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa vyombo vya Habari (MOAT), Dk. Reginald Mengi, aliilaumu tume kushindwa kuvichukulia hatua kali vyama vinavyokiuka maadili ya uchaguzi.

“Tumeshuhudia watu wanatumia lugha za chuki, kutukanana na kukashifiana lakini tume imekuwa ikitoa kauli za jumlajumla badala ya kushughulika na yule aliyekosea,” alisema Dk. Mengi

Akijibu hoja hiyo, Lubuva alisema Tume imekuwa ikipokea malalamiko mengi na imekuwa ikivionya vyama huzika.

Alisema hatua zaidi hutakiwa kuchukuliwa na kamati ya maadili ambayo inaundwa na wagombea wenyewe kitu kinachosababisha kushindwa kukaa mara kwa mara.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Emmanuel Kawishe, alivikumbusha vyombo vya habari kupeleka majina ya waandishi watakaoripoti uchaguzi kwa vile zimeongezwa siku za kuwasilisha majina hadi  Oktoba 5 badala ya Septemba 30 (jana)

“Hadi sasa tumepokea majina 311 na tumefanyia kazi majina 151 na mengine na mengine 160 yanaendelea kufanyiwa kazi na kwa upande wa vyombo vya nje tumepokea majina 11, matano tumeyafanyia kazi na sita yanaendelea kufanyiwa kazi,” alisema Kawishe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles