‘Waliomuua’ Dk. Mvungi waachiwa huru, wakamatwa tena

0
969
Watuhumiwa kesi ya mauaji ya Marehemu Dk Sengondo Mvungi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba wakiwa katika Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana, baada ya kufikishwa na kusomewa mashtaka. Picha na Venance Nestory

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, imewaachia huru watuhumiwa sita wanaodaiwa kumuua kwa makusudi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengodo Mvungi.

Washtakiwa hao wameachiwa huru leo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kuomba kuondoa shtaka hilo kwa kuwa hawana nia ya kuendelea nalo.

Jamhuri ikiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nasoro Katuga, aliwasilisha maombi hayo na mahakama ikakubali kuwaachia washtakiwa hao huru.

Baada ya kuachiwa huru walikamatwa tena na kupelekwa Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka mapya ya mauji ya Dk. Mvungi.

Washtakiwa ni Msigwa Matonya, Mianda Mlewa, Paulo Mdonondo, Longishu Losindo, Juma Kangungu na John Mayunga.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo Novemba 3 mwakasisi 2013 maeneo ya Kibwerenge Msakuzi maeneo ya Mbezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here