27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WALIOMUUA BILIONEA MSUYA WAHUKUMIWA KUNYONGWA

Na UPENDO MOSHA-MOSHI


MAHAKAMA Kuu  Kanda ya Moshi, imewahukumu  washtakiwa watano  kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua aliyekuwa Mfanyabishara wa Madini ya Tanzanite, Bilionea Erasto Msuya.

Pia, mahakama hiyo imemwachia huru mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Shwahibu Jumanne (maarufu kwa jina la Mredi), baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.

Hukumu hiyo ilitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Salma Maghimbi  aliyekuwa akiisikiliza.

Kwa mujibu wa Jaji Maghimbi, ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao watano, ulidhihirisha washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kumuua kwa makusudi Bilionea Msuya.

Katika hukumu hiyo, washtakiwa waliotiwa hatiani na kuhukumia kifo ni mshtakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed, mshitakiwa wa tatu, Musa Mangu, mshitakiwa wa tano, Karimu Kihundwa, mshtakiwa wa sita, Sadiki Jabir na mshtakiwa wa saba, Ally Majeshi.

“Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa dhidi yenu  kwamba kwa pamoja mlikula njama na kufanya nia ovu ya  kumuua mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Erasto Msuya.

“Kwa hiyo, ninawatia hatiani na kuwahukumu wote kunyongwa hadi kufa  lakini mnayo haki ya kukata rufaa.

“Pia, mahakama inamwachia huru mshtakiwa wa pili,  Shahibu Athumani, kwa sababu kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, hakukuwa na ushahidi wa kumtia hatiani na kumuunganisha katika kesi hii ya mauaji,” alisema Jaji Maghimbi alipokuwa akisoma hukumu hiyo  kwa zaidi ya saa moja.

Wakati jaji   akianza kusoma hukumu hiyo, alisema upande wa mashtaka ulikuwa na  mashahidi 27 na vielelezo 26 vya maandishi na vitu vingine huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi wanane na vielelezo vinne vya maandishi.

Inaendelea…………… Jipatie nakala ya Gazeti La Mtanzania

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles