31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Waliokwepa kodi ya vileo waendelea kusota rumande

Kulwa Mzee -Dar es salaam

KESI ya uhujumu uchumi, kukwepa kodi, kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 31.57 na kutakatisha fedha hizo inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Jaruma General Supplies Ltd, Lucas Mallya na wenzake nane, imeendelea kupigwa kalenda.

Kesi hiyo iliahirishwa jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo kwa sababu Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Issaya anayeisikiliza ana udhuru.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kesi hiyo iliyokuja kwa kutajwa, iko mbele ya Hakimu Issaya ambaye amepata udhuru, hivyo aliomba iahirishwe

Hakimu Mwaikambo aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 26 kwa kutajwa.

Mbali ya Mallya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Emmanuel Peter, Happy Mwamugunda, Prochesi Shayo, Prokolini Shayo, Geofrey Urio, Nyasulu Nkyapi, Tunsubilege Mateni na Nelson Kahangwa.

Katika shtaka la kwanza, washtakiwa wanadaiwa kati ya Januari 2015 na Januari 7, 2020 jijini Dar es Salaam, kwa pamoja waliongoza genge la uhalifu kwa nia ya kupata faida.

Inadaiwa shtaka la pili hadi la saba linamkabili Lucas ambaye anadaiwa Juni 3, 2019 Dar es Salaam, alighushi kutengeneza stempu ya ushuru, akionyesha imetengenezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati si kweli.

Anadaiwa alitoa nyaraka hiyo ya kughushi TRA akionyesha ni halali wakati akijua si kweli na katika shtaka lingine inadaiwa Januari 7 mwaka huu, Chang’ombe A, Temeke Dar ee Salaam, alikutwa na rola 93 za stempu zenye thamani ya Sh 80,516,000 alizochapisha bila kibali cha Kamishna wa Mapato.

Lucas anadaiwa kati ya Januari 2016 na Desemba 31, 2019 Dar es Salaam, kwa kutengeneza stempu hizo za kughushi, alisababisha hasara kwa Serikali ya Sh 15,241,075,169, akikwepa kodi kiasi hicho cha fedha na shtaka la saba anadaiwa kutakatisha kiasi hicho cha fedha huku akijua zinatokana na zao la kukwepa kodi.

Mshtakiwa Emmanuel anadaiwa Januari 3 mwaka huu, Mbezi Makabe alikutwa na rola za stempu zenye thamani ya Sh 1,104,000 zilizochapishwa bila kibali cha Kamishna wa Kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles