25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Walioiba mapipa ya madini wafikishwa mahakamani

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

SERIKALI imewafikisha mahakamani watu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la wizi wa mapipa 20 ya mabaki ya madini yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 900.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Mbando na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Jenifa Masue.

Jenifa aliwataja washtakiwa kuwa  ni Jacob Kihombo, Yahaya Masoud, Mbaraka Lipinda, Ramadhani Zombe, Waziri Kibua, Mustapha Mnyika na Richard Sàngana.

Akisoma mashtaka, Jenif alidai washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Februari 6 na 7 mwaka huu  ndàni ya   Dar es Salaam.

Katika shtaka la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa   kula njama ya wizi wa mali inayosafilishwa.

Katika shtaka la pili ilidaiwa  katika tarehe hizo, washtakiwa wote waliiba  mali hiyo ambayo ni mapipa 20 ya mabaki ya madini aina ya Tantalite Concentrates.

Ilidaiwa  madini hayo yana thamani ya Sh 938,339,907 mali ya Kampuni ya Bollore Transport and Logistics.

Shtaka la tatu linamkabili Zombe ambaye ni mlinzi akidaiwa katika tarehe hizo akiwa mwajiriwa wa Kampuni ya Bollore, alishindwa kuzuia kutendeka kwa kosa la wizi wa mapipa hayo ya madini.

Washtakiwa wote walikana mashitaka na  walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana   hadi Aprili 9 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles