24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waliofariki kwa dengue wafikia 13

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Maenfdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema watu waliofariki dunia kwa homa ya dengue ni 13 huku waliougua ugonjwa huo wakiwa 6,677.

Mwalimu alisema hayo jana wakati akizindua wa mkakati wa kupambana na mbu na wadudu wengine, shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Alisema awali takwimu zilionyesha vifo vilikuwa sita lakini Serikali ilifanya tathmini upya na kupata takwimu sahihi.

Alisema katika tathimini hiyo walikuta vifo 13 ambapo Dar es Salaam vipo 11 na wagonjwa 6,631.

Alisema ugonjwa huo kwa sasa unapungua kwani Juni kulikuwa na wagonjwa 536 na tangu Julai hadi jana wagonjwa walikuwa sita pekee.

Alisema homa hiyo ilipoingia watu walipata taharuki na mikakati mipana ya kupambana na ugonjwa huo ikapangwa.

“Ikaonekana bado kuna tatizo kwa kuwa takwimu za Malaria nchini zinaonyesha watu milioni 5.6 milioni wanaugua kila mwaka na vifo 4,390.”

“Sasa tumekuja na mkakati mpana zaidi kupambana na wadudu wadhurifu, wakiwemo mbu, viroboto, chawa, mende, Ndorobo, konokono, kunguni, nzi na papasi,” amesema Waziri Ummy,” alisema.

Alisema Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa asilimia 17 ya magonjwa ya kuambukiza husambazwa na wadudu na kusababisha zaidi ya vifo millioni moja kila mwaka.

“Kwa mfano, malaria peke yake inakadiriwa kusababisha vifo 400,000 kila mwaka na wengi wanaofariki ni watoto chini ya miaka mitano. Aidha, inakadiriwa kuwa zaidi ya watu billion 2.5 kutoka katika nchi 100 ikiwemo Tanzania wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa homa ya Dengue,” alisema.

Ummy alisema zaidi ya asilimia 94 ya Watanzania wanaishi katika maeneo yenye mbu wa malaria.

Hata hivyo alisema uwekezaji wa Serikali, umesaidia kupungua kwa kiwango cha malaria kutoka asilimia 18.1 mwaka 2008 hadi asilimia 7.3 ya sasa.

Alisema kutokana na kuendelea kujitokeza kwa magonjwa yaenezwayo na wadudu, Wizara imeandaa mkakati wa kudhibiti mbu na wadudu wengine wadhurifu.

“Lengo ni kuhakikisha tunadhibiti mbu na wadudu wengine wadhurifu kwa njia ya utengamano na kwa kuhakikisha jamii inashiriki kikamilifu kupambana na wadudu hawa wadhurifu.

“Katika kuimarisha udhibiti huu wizara imeagiza mashine zenye uwezo wa kupulizia nane zinazobebwa na magari na kupuliza eneo kubwa kwa wakati mmoja na tayari mashine nne zimeisha wasili hapa nchini.

“Mashine mbili kati ya nne zilizopo zitaanza kutumika Dar es Salaam kwakuwa kuna idadi kubwa ya wagonjwa. Mashine moja itapelekwaTanga ambapo kuna wagonjwa wengi wa dengue pia.

“Aidha, kwa kuzingatia mwingiliano mkubwa watu Makao Makuu ya Serikali Dodoma mashine ya nne itapelekwa mkoa huo na ikimaliza kazi itapelekwa mikoa mingine,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles