33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Walioambukizwa corona Kenya wafika 246

 NAIROBI, KENYA 

KENYA imethibitisha wagonjwa wapya 12 wa corona na kufikisha jumla ya watu walioambukizwa 246.

Kenya imetangaza idadi hiyo ya wagonjwa wa corona baada ya kuthibitisha wengine wapya 12 walioambukizwa virusi hivyo.

Katika taarifa ya Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe, amesema watano kati ya wale walioambukizwa virusi vya corona ni wahudumu wa hoteli na kuongeza kuwa idadi hiyo ilifikiwa baada ya jumla ya sampuli 400 kufanyiwa uchunguzi.

Juzi Rais Uhuru Kenyata alitangaza hatua kadhaa za kukabiliana na Covid-19.

Hatua hizo ni pamoja na Wizara ya Afya na huduma za umma kuanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19.

Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takriban miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.

Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitafaidi kutokana na fedha zilizotengwa na Serikali kusaidia familia zisizojiweza.

Aidha alisema Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.

Ili kuhakikisha msaada unagawanywa kwa njia salama, mfuko wa hali ya dharura wa kukabiliana na Covid-19, Kenya na mashirika mengine ya usalama yatashirikiana kuratibu miradi kama ule wa Adopt a Needy Family, ambapo raia wa Kenya wasio na uwezo watasaidiwa katika kipindi hiki cha janga kuhakikisha hatua zinachukuliwa bila kufuata urasimu.

Aidha ofisa yeyote wa polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.

Kenya imepokea karibu vifaa 40,000 vya kupimia Jumatano wiki hii ikiwa ni katika kuimarisha hatua za kuimarisha uwezo wa kupima watu kunakoendana na lengo la kupimana kutengwa wale walioathirika.

Wizara ya afya ilitangaza Jumatano kwamba nchi hiyo imepokea vifaa vya kupimia mfano wa vijiti 18,900, vifaa vya kuwekea vipimo 18,912, sare na vifaa vya kujikinga kwa wahudumu wa afya vipimajoto vya kushikiliwa, glavu na mashine za kupuma kutoka kwa mfanyabiashara wa kundi la Alibaba, Jack Ma.

Waziri amesema Kenya pia ilikuwa imepokea shehena ya glavu, vifaa vya kujikinga kwenye uso na barakoa zinazovaliwa wakati wa upasuaji kutoka China, Ufaransa na Ujerumani kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO).

MATAIFA AFRIKA YAPATA VIFAA MILIONI MOJA VYA KUPIMIA 

Wakati huo huo mataifa ya Afrika yatakabidhiwa jumla ya vifaa milioni moja vya kupimia ili kuyasaidia kwenye vita dhidi ya mripuko wa kirusi cha corona. 

kwa mujibu wa Kituo cha Kukabiliana na Maradhi cha Afrika, CDC, Mkurugenzi wa kituo hicho, John Nkengasong, amesema kuna pengo kubwa barani Afrika hasa kwenye suala la vipimo, huku akisisitiza kuwa kunahitajika angalau vipimo milioni 15 ndani ya kipindi cha miezi mitatu hadi sita ijayo kutoka sasa. 

Ujerumani imekipatia kituo cha CDC vifaa hivyo milioni moja, ambavyo vitaanza kusambazwa wiki ijayo, kwa mujibu wa kituo hicho. 

Kufikia asubuhi ya juzi, Alhamisi, CDC ilikuwa imesharekodi wagonjwa 17,200 waliokwishaambukizwa kirusi cha corona, ambapo 1000 wamepoteza maisha katika mataifa 52 kati ya 54 barani Afrika. 

Hadi sasa ni mataifa mawili tu ya bara hilo ambayo hayajaripoti mgonjwa hata mmoja wa COVID-19

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles