30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WALIMU WALIOWAPA UJAUZITO WANAFUNZI KUSAKWA

Na TIMOTHY ITEMBE, RORYA


MKUU wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Simion Chacha, amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Charles Chacha, kuwachukulia hatua za kisheria ikiwamo kuwafukuza kazi walimu wanaodaiwa kuwapa ujauzito wanafunzi.

Agizo hilo alilitoa juzi katika kikao cha baraza la madiwani kuhusiana na msimamo wa Serikali kwa wanafunzi ambao wanapata  ujauzito shuleni kwamba  hawana nafasi ya kuendelea na masomo na kuwataka wananchi kuungana na Serikali kupiga vita vitendo hivyo ili visiendelee kutokea.

Mkuu huyo wa wilaya alisema amepata  tetesi kuwa kuna walimu kutoka Shule ya Msingi Nyamugere na Kirogo wanadaiwa kuwapa mimba wanafunzi wao, lakini cha kusikitisha  hatua za kiuchunguzi hazijachukuliwa ili kubaini ukweli.

“Mimi nitoe agizo kwako wewe mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya ili ukawachukulie hatua walimu hao ambao wanadaiwa kuwapachika mimba wanafunzi wao shuleni, hatutaki kulea watu kama hao na kuwafukuza kazi itakuwa fundisho kwa wengine,” alisema Chacha.

Naye Diwani Kata ya Bukwe, Charles Wembe (CCM), alisema halmashauri hiyo kupitia madiwani wake wanatakiwa kuwa chachu kwa kutoa elimu na kusimamia sheria.

“Watoto wetu wanaharibiwa na baadhi ya walimu ambao si waaminifu, sasa  kwa hali hiyo tunatakiwa kusimamia haki pasipo kuwatetea wahalifu,” alisema Wembe.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya, Chacha, alisema baadhi ya wazazi na walezi wa watoto  wanaficha ukweli pale inapotokea kitendo  huku wahusika wakikubaliana  mitaani, ambapo kesi inapofikishwa mahakamani hukosa ushahidi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles