30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Walimu shule binafsi wadai kusitishiwa mishahara yao

Yohana Paul – Mwanza

CHAMA Cha Waalimu wa Shule Binafsi (TPTU), kimeiomba Serikali kuwachukulia hatua, ikiwamo kuwafungulia mashtaka ya uhujumu uchumu wamiliki wa shule binafsi ambao wamewasitishia mishahara na ajira wafanyakazi wao hasa walimu wakati huu likizo ya janga la ugonjwa wa corona.

Akizungumuza na waaandishi wa habari juzi jijini Mwanza, Rais wa TPTU, Cornel Bupolo alisema mpaka sasa amepokea taarifa kutoka kwa wanachama wake walio  maeneo tofauti wakilalamika kusitishiwa mishahara yao mara tu,  baada ya Serikali kuamuru vyuo na shule zote kufungwa kupisha janga la virusi vya corona.

Alisema pamoja na kisingizio hicho pia wapo baadhi ya wamiliki wa shule binafsi, wameripotiwa kutolipa mishara kwa walimu wao toka shule zilipofunguliwa Januari, mwaka huu hali ambayo imewafanya walimu kuendelea kuishi maisha magumu kwa kukosa fedha za kujikimu.

Alisema Serikali inapaswa kufuatilia kwa ukaribu  wamiliki wa shule binafsi,wengi wao suala la kutokulipa mishahara kwa miezi mitatu na zaidi imekuwa kasumba yao ya muda mrefu hata kabla ya janga hili.

“Ni aibu kubwa  kwa mwajiri au mmiliki wa shule aliyeomba usajili na akapatiwa na Serikali,eti akapata tatizo kwa muda wa mwezi mmoja akaanza kulia, hii ni aibu kubwa, niiombe serikali iwafuatilie kwa ukaribu sana hawa watu kwa kuwa haiwezekani wanaendelea kupokea ada na michango ya wanafunzi harafu wasilipe mishahara huo ni uhujumu uchumi.

“Hawa watu ukitafakari makosa wanayoyafanya hawa wamiliki wa shule ni wahujumu uchumi kama wahujumu uchumi wengine wanaokamatwa na serikali kwa sababu haiwezekani, unaendelea kufanyisha watu kazi na unajiingizia kipato harafu hutaki kulipa mishahara wafanyakazi wako, wewe ni mhujumu uchumi.

“Rais ameendelea kuwasisitiza Watanzania kufanya kazi kwa weledi ili kulipa kodi,sisi TPTU tumebaini watu wanafanya kazi, hawalipi mishahara wengine tangu Desemba, mwaka jana mpaka sasa tunavyozungumuza hawajawalipa walimu mishahara harafu eti wameachwa wanazunguka mitaani, tunaomba washughulikiwe,” alisema Bupolo.

Katibu Mkuu wa TPTU, Julius Mabula alisema changamoto ya  walimu haijaishia tu kutolipwa mishahara, bali tatizo limeenda mbali, baada ya likizo ya awali ya kupisha janga la corona kwa siku 30 kutangazwa waajiri wengine walianza kuwasitishia walimu mikataba pasipo utaratibu maalumu.

Alisema baada ya serikali kutoa la kufungwa kwa shule na vyuo kwa muda usiojulikana tatizo la kusitisha mikataba na mishahara, limekuwa kubwa kwa kuliona hilo,wameamua kulisimamia kidete jambo hili kwani wamesajiliwa kisheriani wakiwa na majukumu makubwa matatu kwa maana ya kusimamia haki za waalimu, maslahi ya waalimu na usalama wa waalimu kwenye maeneo yao ya kazi.

“Kwenye hili suala, NSSF wanatakiwa watimize majukumu yao pia kwa kukusanya hayo makato kutoka kwa wamiliki wa shule kwani makato  haya ndio akiba ya waalimu kwa baadaye itakayowasaidia kujikimu pale nguvu zitakapokuwa zimewaishia kwa maana hiyo NSSF wafanye ukaguzi shule kwa shule kubaini tatizo hili,” alisema Mabula.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,352FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles