‘Walimu msiwasuse wanafunzi wenye uelewa mdogo’

0
886

AMON MTEGA-SONGEA

WALIMU wametakiwa kuacha tabia kuyasusia madarasa yenye wanafunzi wanaodaiwa kuwa na uelewa mdogo kitaaluma na badala yake waongeze mbinu ya kuwafundisha zaidi.

Wito huo umetolewa jana na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea,Daniel Zake, wakati mahafali ya 31  kwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Legele iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Alisema kuwa kunatabia imejengeka kwa baadhi ya walimu, kuyasusa madarasa yanayodaiwa kuwa wanafunzi wenye uelewa mdogo jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa baadhi ya wanafunzi kujikuta wakitaka tamaa.

Meneja huyo ambaye alikuwa mgeni rasi katika mahafali hayo, alisema kuwa hatua hiyo hawezo kusaidia kukuza elimu bali itadidimiza na watoto kujikuta hawezi kujifunza sawasawa kutokana na kususwa na walimu wao.

“’Walimu lazima watafute mbinu za kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu na siyo kususia kuwa wanafunzi hawa hawaambiliki hawasikii jambo ambalo halitakiwi,” alisema Zake.

Alisema kuwa Serikali imewaamini kuwapatia ajira hivyo ni vema wakaitendea haki ya kutumia maarifa yao ya kuwafund9sha wanafunzo hao kwani ndio viongozi wajao wa taifa.

Awali kwaakisoma risala ya wahitimu shule hapo, Avitho Mtega, alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa vyumba vya madarasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here