25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘WALIMU ELIMU YA AWALI WANATUMIA UZOEFU KUFUNDISHA’

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


VYUO vingi vinavyotoa mafunzo kwa walimu wa shule za awali nchini havitoi mafunzo ya namna ya kufundisha masomo kwa watoto wadogo na kusababisha walimu hao kufundisha kwa kutumia uzoefu.

Akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za awali iliyofanyika Dar es Salaam juzi, Mratibu wa semina hiyo, Kelvin Shola, alisema vyuo vingi nchini vinafundisha namna ya kuwalea watoto kuliko wanavyopaswa kufundisha masomo.

Alisema  hali hiyo imechangia kuwapo na tatizo la walimu wengi kushindwa kutumia mtaala wa elimu ya awali na kushindwa kufahamu nini anachopaswa kufundishwa motto, jambo linalosababishwa watoto kufundishwa mambo makubwa yasiyoendana na umri wao.

 “Moja ya matatizo tuliyonayo ni kutokuwa na walimu wanaomudu masomo husika kama hesabu, badala yake walimu wanatumia uzoefu wao kufundisha,” alisema Shola.

Mmoja wa walimu waliohudhuria semina hiyo, Agness Mringo, alisema imemsaidia kufahamu eneo lipi anapaswa kuongeza bidii, hivyo anaamini atabadili mfumo wake wa ufundishaji aliokuwa akitumia awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles