28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

WALIMU BUNDA WAKIMBIA UHAKIKI WA VYETI

Na AHMED MAKONGO-BUNDA

BAADHI ya walimu katika shule za msingi katika Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara, wamekimbia vituo vyao vya kazi wakikwepa zoezi la uhakiki wa vyeti.

Akizungumza juzi wakati wa kikao cha kazi cha Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Janeth Mayanja, alisema baadhi ya walimu wa shule za msingi wakati wa zoezi la uhakiki wa vyeti, lililoendeshwa na serikali walitoroka kweye vituo vyao vya kazi na kushindwa kuhakikikiwa.

“Tunawafuatilia waliotoroka na ndiyo maana tunajua baadhi wamekwisha rejea, wanapaswa kutambua zoezi la uhakiki wa yeti halijaisha lipo palepale na kukimbuia wanajidanganya kwa sababu lazima tutawahakiki,” alisema Mayanja.

Alisema kufuatia walimu hao kukimbia walimu wakuu wa shule ambao walimu wao walikwepa kuhakikiwa au hawakuwepo wakati wa zoezi la uhakiki, wametakiwa kuandika majina na taarifa sahihi juu ya walimu hao ili waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

“Andikeni majina ya walimu wote waliotoroka wakati wa zoezi hilo na kulezileta kwetu…, ila walimu wakuu watakaoshindwa kufanya hivyo wajue nao watageuka kuwa majipu,” alisema Mayanja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mayaya Magesse aliwataka walimu kufanya kazi kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati sahihi.

Alisema baadhi yao wamekuwa wakikwepa kufika kazini kwa visingizio mbalimbali vya kuumwa kwa ajili ya kufanya mambo yao, hivyo kuwaonya kuwa wanakabiliwa na hatua za kupoteza ajira zao iwapo watabainika na kuthibitishwa kwa makosa husika.

Naye Ofisa Elimu taaluma kwa Shule za Msingi katika Halmashauri ya Mji wa Bunda, Reuben Kaswamila, alisema kuwa kikao hicho ni cha kazi kwa ajili ya kuboresha elimu na kubadilishana mbinu na maarifa kwa baadhi ya walimu ambao shule zao zimefanya vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles