23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Walimu 500 kujadili ukatili kwa watoto shuleni,nyumbani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shule za Rightway, kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la Mine Foundation pamoja na wadau wengine wa elimu wameandaa kongamano kubwa la walimu likijumuisha walimu wa shule za msingi na sekondari za Serikali na binafsi ili kuzungumzia changamoto ya ukatili kwa watoto.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe 15 Desemba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari, Muasisi na Mkurugenzi wa shule za Rightway, Mercy Mchechu alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kushirikishana mbinu mbali mbali za kuwalinda watoto dhidi ya ukatili hasa wakiwa maeneo ya shuleni.

“Sisi sote kwa pamoja tuna wajibu wa kutafuta ufumbuzi na kushughulikia sababu za unyanyasaji huu shuleni na nyumbani ili kuhakikisha watoto wanalelewa kwenye mazingira salama,” alisema Mercy.

Utafiti uliofanywa na shirika la HakiElimu mwaka 2020 ulibaini uwepo mkubwa wa matukio ya unyanyasaji wa watoto katika mifumo tofauti.

Takribani asilimia 87.9 ya watoto wote waliosailiwa, wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili, hususani kupitia adhabu za viboko, asilimia 17.0 ya watoto walio shule za umma na asilimia 14.3 walio shule binafsi wamewahi kunyanyaswa kingono angalau mara moja, wakati asilimia 34.3 ya watoto wa shule kwa ujumla wamenyanyaswa kisaikolojia hasa na wazazi au walezi.

“Walimu wana nafasi kubwa ya kukomesha vitendo vya kikatili dhidi ya watoto mashuleni ikiwa watashirikishwa kwa kupewa taarifa sahihi na mbinu za kutumia ili waweze kuwajengea watoto uwezo wa kutambua ukatili na kuutolea taarifa pindi tu utakapojitokeza na hili ndio lengo kuu la kongamano hil,” aliongezea Mercy.

Naye Mdau wa Shule za Rightway na Meneja wa Mine Foundation, Joab Ndanzi alisema kuwa mada na mijadala katika kongamano hilo itaendeshwa na wataalamu kutoka polisi dawati la jinsia, ustawi wa jamii, shirika la HakiElimu na wadau wengine.

Kongamano hili la siku moja kuanzia saa mbili asubuhi, litafanyikia katika ukumbi wa Oasis Village ulioko Mbezi Beach Beach jijini Dar es Salaam na kukutanisha walimu zaidi ya mia tano kutoka mikoa mbalimbali Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles