24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WALETA MABADILIKO WANAVYOGUSA MAISHA YA WATOTO, WANAWAKE

Na MWANDISHI WETU


KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Reach for Change  imetoa tuzo ya Dola za Marekani 20,000 kwa kila mmoja kwa washindi wawili  wa shindano la tano  la Kidijitali la Tigo la waleta mabadiliko (Tigo Digital Changemakers).

Shindano hilo  linalenga  kuibua na kuwasaidia wajasiriamali jamii  ambao wanatumia programu na teknolojia katika kuboresha  jamii na kuleta mabadiliko kwa vizazi vijavyo.

Pamoja na nyongeza katika msaada huo wa kifedha, washindi  wanapewa nafasi ya kutumia  kituo cha  Reach for Change ambacho kinawapatia ushauri, utaalamu na  kuingia katika mitandao duniani ambayo itawawezesha kujenga ujasiriamali jamii  ulio endelevu kifedha utakaounda mabadiliko katika uwanja mpana.

Washindi wa mwaka huu katika tuzo hiyo ni Sophia Mbega  na Nancy Sumari. Sophia Mbega aliwavutia majaji  na mkakati wake mkubwa wa kidijitali  ambao umejielekeza katika  kuvisaidia  vikundi binafsi vya wanawake  maarufu VICOBA. Ameibuka na programu ya simu  ambayo inaunda  jukwaa la ushirikiano  linalotumia programu zilizopo kwa usimamizi wa kifedha na majukumu  katika njia ambayo  inaendana na mazingira ya Kiafrika. Kupitia programu hiyo, watumiaji wote, bila kujali sehemu wanayokuwapo  wanaweza kuhamisha fedha  kwenda katika akaunti  ya kikundi cha Vicoba (ikiwa ni moja kwa moja  kwa kutumia namba iliyo katika mfumo wa USSD), kuangalia rekodi zao zote za kifedha, faida iliyozalishwa, taarifa za wiki n.k.

Mkakati ulioshinda tuzo wa Nancy Sumari  unaitwa Kids Jenga Hub ambao unaangalia msingi wa uelewa wa watoto.  Kupitia mkakati huo wa  nafasi ya kuanza kuwashirikisha  watoto, anafundisha  programu za kompyuta, matumizi ya kiroboti  na stadi za kuweka namba  kwa wanafunzi wa  shule ya msingi.  Mkakati huo pia unawafunulia watoto katika kujifunza msingi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kama vile  stadi za kiprogramu ambazo matokeo yake  zinatumika katika malengo mengi ya kielimu na burudani.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  anasema; “Ni kutokana na furaha hii kubwa, tunatangaza washindi  wa mwaka huu wa shindano la Tigo la kidijitali la waleta mabadiliko. “Kwa mwaka wa tano sasa waleta mabadiliko wameyagusa maisha ya watoto zaidi ya 250,000 nchini Tanzania  na tunaamini kwamba kwa nyongeza hii ya waleta mabadiliko wawili  tutaleta mabadiliko  katika maisha ya watoto wengi zaidi na kusaidia kuifanya Tanzania  kuwa sehemu nzuri kwa  vizazi vyetu vijavyo.”

Gutierrez anafafanua kuwa  kama nembo ya maisha ya kidijitali, Tigo inatoa msukumo kwa mawazo na miradi inayoendeshwa  na teknolojia  ambayo yanaleta mabadiliko endelevu.

“Teknolojia ya kidijitali si tu inabadilisha namna ambavyo tunafanya  biashara ndani ya Afrika  bali pia  inaleta mapinduzi  kwa njia tofauti  na  kutatua masuala ya maendeleo ya jamii.

“Hivyo, kutokana na heshima hii kubwa  ni kwamba kwa mara nyingine tunaunda fursa kwa  kwa mawazo hayo kutambuliwa, kuungwa mkono na kubadilisha hadi kiwango cha juu cha matokeo ya kijamii na kiuchumi,” anasema.

Huu ni mwaka wa tano  ambapo Tigo  na Reach for Change  wanatangaza washindi wa shindano hilo. Washindi walioingia fainali ambao huchaguliwa kutoka kundi la mamia ya  wajasirimali jamii  ambao wametumia programu za  kiteknolojia hupata suluhisho  kwa matatizo yanayoikabilia jamii ya Watanzania.

Gutierrez anawapongeza washindi waliotangulia na papo hapo akitoa msukumo kwa  wengine kushirikiana mawazo yao.

 “Uchaguzi wetu wa wajasiriamali jamii unavutia mno. Hadi sasa  tumeshasaidia jumla ya waleta mabadiliko ya kidijitali jamii tisa na tunatarajia kuwasaidia  wajasiriamali jamii wengine  kila mwaka,  ili kufanya karakati hizi zisonge mbele,”anasema.

Waleta mabadiliko katika programu hii ni pamoja na Faraja Nyalandu ambaye anaendesha  ujasiriamali jamii  kidijitali  unaofahamika Shule Direct. Shule Direct  inatoa mada za kielimu  kidijitali  kukabiliana na uhaba wa walimu na kuhakikisha  kila mtoto na  vijana wanapata elimu bora. Asasi ya Faraja pia inatoa  programu ya simu  inayoitwa Makini SMS ambayo inawasaidia watoto kujifunza  kwa kutumia maswali ya kuchagua masomo tisa. Hivi sasa  amepanga kuifanya  asasi hiyo kuwa ya kikanda.

Carolyne Ekyarisiima ni mleta mabadiliko ya kidijitali mwingine wa Tigo ambaye anafanya kazi ya  kuziba pengo la kijinsia katika  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia  ujasiriamali wake wa kijamii, Apps & Girls. Carolyne  ameleta mabadiliko kwa mamia ya watoto wa kike, kupitia  klabu za masomo shuleni, warsha, maonesho, kuweka kambi pamoja  na mashindano. Si tu kwamba hii inasaidia  bali pia  inahakikisha  kwamba watoto wa kike wengi  wanaweza kuzifikia  teknolojia za kidijitali. Hali kadhalika Carolyne amewawezesha kuwa  viongozi wa Tehama wa baadaye. Carolyne  hivi sasa anaupanua ujasirimali jamii wake  kuleta matokeo makubwa na kuwapatia wasichana walio wengi  elimu ya teknolojia  na kuwasaidia kuanzisha suluhisho  kwa masuala ya kijamii  kupitia programu zao za  kidijitali  na mitandao.

Joan Avit naye ni mleta anayeboresha  ubora wa elimu ya awali  kupitia ubunifu wa  kidijitali. Ubunifu wake unaofahamika GraphoGame  Tanzania unawawezesha watoto kujifunza kupitia mchezo ambao ni rafiki kwao… unawasaidia kujifunza kusoma  kwa kuzitambua  herufi. Ubunifu wake umebadilisha maisha kwa mamia ya wanafunzi wadogo ambao awali walikuwa na hali mbaya katika kujifunza lakini hivi sasa wanachanua kutokana na  ubunifu wa kidijitali.

 “Tumekuwa tukiunga mkono kazi zote za waleta mabadiliko wetu  na mwaka huu  tumeangalia na kuwaunga mkono wajasiriamali jamii wengine wawili walio jasiri na wabunifu,” anasema Gutierrez.

Akizungumza katika hafla ya tuzo hiyo, Meneja Programu  wa Reach for Change Tanzania Josephine Msambichaka alipongeza  ushirikiano wa asasi  hiyo na Tigo, akibainisha kwamba imetoa  fursa sahihi kwa utekelezaji wa  miundo ya biashara iliyoendelevu ambayo inanufaisha jamii  hususani  idadi kubwa ya watoto kote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles