Na FARAJA MASINDE
HAKI za watu wenye ulemavu zinalindwa katika mikataba mbalimbali ya haki za binadamu, hususan Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu (CRPD) wa mwaka 2006, ambao Tanzania imeuridhia.
Mwaka 2010, Tanzania ilitunga sheria ya watu wenye ulemavu, inayoendana na mkataba huo. Sheria hii pia inalinda haki za watu wenye ulemavu, ikiwamo haki ya kutobaguliwa, kufanya kazi, kupata ajira, haki ya elimu, haki ya usawa mbele ya sheria na haki ya afya.
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu unazitaka serikali kuchukua hatua kadhaa ili kulinda haki ya watu wenye ulemavu ya kufanya kazi, ikiwamo:
Kukataza ubaguzi wa watu wenye ulemavu katika masuala ya ajira; kulinda haki za watu wenye ulemavu sawa na watu wengine, ikiwamo mazingira bora ya kazi na kuwalinda dhidi ya ukatili; kuhakikisha watu wenye ulemavu walioajiriwa wanaweza kufurahia haki ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi sawa na wafanyakazi wengine na kuweka sera na mikakati ya kuimarisha nafasi za ajira kwa watu wenye ulemavu kwenye sekta binafsi.
Sheria hii inalenga kutekeleza sera ya taifa ya ulemavu ya mwaka 2004 na inampa mamlaka waziri mwenye dhamana kwa kushirikiana na waziri mwenye dhamana ya kazi, kutunga kanuni zinazowataka waajiri wenye wafanyakazi 20 na zaidi kuhakikisha kati yao asilimia 30 ni watu wenye ulemavu.
Lakini pia, sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 inakataza ubaguzi katika ajira na mahala pa kazi, ikiwamo ubaguzi dhidi ya watu wenyeulemavu.
Ripoti ya hivi karibuni ya Haki za Binadamu na Bishara Tanzania bara ya mwaka 2018/19 ya kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) imefichua namna ambavyo watu wenye ulamavu pamoja na wale wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi wanavyowekwa kando kwenye ajira.
Imeripotiwa kuwa kutengwa kwa watu wenye ulemavu mahali pa kazi, kwa njia ya ubaguzi au mazingi magumu ya kazi imegharimu Tanzania dola milioni 480 kila mwaka ambayo ni sawa na asilimia 3.76 ya pato la taifa.
Kama inavyofahamika kwamba watu wenye ulemavu mara nyingi uishi katika umaskini mkubwa kwa sababu ya changamoto ya kupata kipato cha kutosha kutokana na kutengwa na watu wengi.
Kati ya watu hao ni asilimia 3.1 tu ndiyo kupata mapato kutokana na kazi inayolipwa, inaonyesha kuwa, kaya zenye watu wengi wenye ulemavu zinaongoza kwakuwa na kiwango kikubwa cha umaskini.
Pamoja na uwapo wa sheria na kanuni zinazowalinda, bado wanaendelea kukumbwa na changamoto na ubaguzi wa aina mbalimbali.
Baadhi ya changamoto zinazowakumba watu hao kwenye sekta ya ajira ni pamoja na ukosefu wa elimu, kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na jambo fulani, unyanyasaji, utekelezaji mdogo wa sheria zinazosimamia haki za watu wenye ulemavu.
Pia kuna ukosefu wa miundombinu madhubuti inayoendana na hali yao, kunyimwa nafasi za ajira hata pale ambapo wanaweza kupatiwa fursa hizo.
Hilo ni jambo ambalo linaweza kusababisha faini isiyopungua milioni mbili au kifungo kisichozidi mwaka mmoja, au vyote.
“Utafiti umebaini kuwa waajiri wengi hawataki kuajiri watu wenye ulemavu kwa kigezo kuwa hawana uwezo wa kufanyakazi na watachelewesha matokeo ya haraka ya ufranyajikazi.
“Wafanyakazi wanaokumbwa na ulemavu wakiwa kwnye maeneo yao ya kazi wengi wao huachishwa kwa kigezo kuwa uwezo wao wa kufanyakzi hautakuwa sambamba na mtu asiye na ulemavu.
“Hivyo basi, ubaguzi wa watu wenye ulemavu katika kupata ajira bado ni changamoto kubwa, ubaguzi wa watu wenye ulemavu katika kupata ajira bado ni changamoto kubwa, makampuni mengi yaliyofikiwa yalionekana kutozingatia sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 inayotaka asilia 3 ya wafanyakazi walioajiriwa wawe watu wenye ulemavu,” inaeleza ripoti hiyo.
Kundi la watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi ni mojawapo ya makundi yanayohitaji ulinzi na uangalizi maalumu.
Ripoti hiyo inasema watu hao wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali katika jamii na mahala pa kazi, hasa ubaguzi na unyanyapaa.
“Sheria ya Kuzuia na Kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2008 inalinda haki za watu wanaoishi na Ukimwi na kukataza ubaguzi na unyanyapaa dhidi yao.
“Sheria hii inasisitiza kwamba watu wanaoishi na VVU wasibaguliwe mahala pa kazi na katika kutafuta ajira. Kwa mujibu wa sheria hii, ni kosa la jinai kuwabagua na kuwanyanyapaa watu wa aina hiyo,” inabainisha ripoti hiyo.
Sheria ya Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 nayo inakataza ubaguzi dhidi ya wafanyakazi kwa sababu ya kuwa na virusi vya pale ambapo mfanyakazi akiweka wazi hali yake ya kwamba ana VVU kwa mwajiri wake basi mwajiri anapaswa kumlinda ubaguzi dhidi ya na unyanyapaa.
Kuwe na mazingira ambayo hayataruhusu unyanyapaa na ubaguzi wa mfanyakazi anayeishi na VVU kutoka kwa wafanyakazi wenzake.
“Mojawapo ya kampuni zilizotembelewa na utafiti ambao ulihusisha mikoa 15 ya Tanzania bara, ilikutwa mkataba ambao unawabagua watu wenye VVU kwa kueleza kwamba mfanyakazi atakapogundulika ana virusi hivyo basi ataachishwa kazi,” inaeleza ripoti hiyo.
Lakini pia, inafafanua kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakipitia mazingira magumu zaidi kazini kwani moja ya watu waliofanyiwa mahojiano kwenye ripoti hiyo walieleza kuwa hulazimika kukatwa asilimia 300 ya mshahara wao pale ambapo wanakuwa hawajafanyakazi kwa sababu zinazokubalika na mwajiri, jambo ambalo huwalazimu kufanya kazi kwa miezi mitatu bila mishahara.
“Kama itatokea mfanyakazi amepata maradhi kama Kifua Kikuu, VVU na mengine, kampuni itavunja mara moja mkataba wake,” inaeleza ripoti hiyo.