27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WALAANI MATUMIZI  VIUNGO VYA ALBINO KUPIGIA RAMLI

Na Samwel Mwanga


WAGANGA wa tiba asili wilayani Busega wamekemea tabia ya baadhi ya wenzao wanaotumia viungo vya  albino   kupiga ramli.

Wamependekeza watu wa aina hiyo  wakikamatwa wanyongwe hadharani bila kufikishwa mahakamani.

Mapendekezo hayo yalitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Tiba asili wilayani humo, Peter Magubu,  katika mkutano wa wanachama wa chama hicho.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuhakikisha vitendo vya kuuawa albino vinatokomezwa katika Wilaya ya Busega.

Alisema    njia nyingine ya kutokomeza vitendo hivyo ni pamoja na serikali kuhakikisha inawasajiliwaganga wote wa tiba asilia.

Magubu alisema hatua hiyo itarahisisha  kuwatambua ni yupi anayejihusisha na   ukatili wa namna hiyo  aweze kuchukuliwa hatua kali za  sheria.

Alisema kwa sasa matapeli ni wengi ambao wamevamia na kufanya shughuli hizo kwa lengo la kutaka kujipatia fedha.

Alisema kwa sababu hiyo   inabidi serikali isiwafumbie macho kwa sababu hakuna ukweli wowote kuhusu jambo

hilo la viungo vya  albino kuwatajirisha watu.

“Tunaiomba serikali iwanyonge watu hao wanaobainika kutumia viungo hivyo vya binadamu wenzetu   iwe fundisho kwa walio na imani hizo za kijinga,” alisema.

Mratibu Mkuu wa Wilaya wa Tiba asili, John Balele aliwaomba waganga  wote  wa chama hicho   na wale wasio wanachama wilaya humo kuonyesha umoja na mshikamano.

Alisema hiyo itakuwa ni katika kuhakikisha wanakomesha jambo hili la udanganyifu wa matumizi ya viungo vya  albino  nchini.

 “Kwa sasa serikali inatakiwa kupiga marufuku   vituo vya kuwalea  albino   jamii iweze kukaa nao  majumbani.

“Wnapozidi kukaa katika vituo  hivyo   wanajionakutengwa jambo ambalo linawafanya kutokuwa na amani,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles