26.1 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wakuu wa polisi Afrika Mashariki kudhibiti uhalifu wa kuvuka mipaka

Janeth Mushi, Arusha

Wakuu wa Majeshi ya Polisi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wametia saini makubaliano ya namna bora ya  kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka (Cross Border Organized Crimes), ili kupunguza matukio hayo.

Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na dawa za kulevya, ugaidi pamoja na kusafirisha binadamu isivyo halali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amesema kutokana na masuala hayo kuhusisha mipaka, nchi moja moja haziwezi kuyashughulikia ndiyo maana wameamua kuungana na kushirikiana ili kutokomeza uhalifu unaovuka mipaka.

“Moja ya masuala tuliyojadiliana kwa kina juu ya dawa za kulevya aina ya mirungi ambayo inaruhusiwa Kenya ila ni makosa katika nchi nyingine wanachama ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda.

“Namna ya kuweza kupambana nayo ni lazima kuna vitu tukubaliane, mambo ambayo yamezungumzwa namna gani tuboreshe sheria zetu na adhabu zikawa zinafanana,” amesema Sirro.

Kutokana na hali hiyo, amesema wameomba wenzao wa Kenya ni namna gani wanaweza kurekebisha sheria, zikalingana na nchi nyingine za EAC ili ikiamuliwa hili ni kosa mirungi iwe kosa nchi zote, ili kuwe sawa kote.

IGP Sirro amesema jambo lingine waliloangalia maabara kubwa kwamba lazima zifanye kazi kwa pamoja kwa kuwa na taratibu na kanuni moja hivyo kikao kimeelekeza wakuu wa maabara hizo za nchi wanachama ni vema wakakutana wakaziandaa kwa pamoja, zikapitiwa kisha kupelekwa kwa mawaziri zifanyiwe kazi.

“Kuna mambo mengi tumekubaliana ambayo yakitekelezwa yatasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa sana haya makosa ambayo yanavuka mipaka, tunashukuru sekretarieti ya EAC, kwani mipaka imewekwa tu na wenzetu ila isifanye tusifanye kazi pamoja, uhalifu hauna mikapa na sisi hatuna sababu ya kuwa na mipaka lazima tushirikiane,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles