30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAKUU WA IDARA KITETO WAONYWA

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona.

Na MOHAMED HAMAD,

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona, amesema hatawavumilia watumishi wa Serikali wilayani humo watakaoshindwa kutimiza wajibu wao.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi ya ujenzi na umwagiliaji yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 400 juzi, Kambona alisema baadhi ya wakuu wa idara hawatimizi wajibu wao na kwamba njia pekee ni kuwachukulia hatua za kinidhamu.

“Kuna watu wanashindwa kutimiza wajibu wao wakati wao ni watumishi wa umma. Katika hili, nitaanza na ofisa kilimo wa wilaya ambaye ameshindwa kuwajibika na kusababisha manung’uniko kwa wananchi.

“Watu kama hawa hatuna sababu ya kuwa nao humu, tumesema kila mtumishi awafikie wananchi walipo.

“Lakini jambo la ajabu ni kwamba, tangu tuzindue mradi wa maji zaidi ya mwezi, katika Kijiji cha Orgira, hajautembelea mradi huo ili kuona kinachoendelea wakati akijua umegharimu zaidi ya Sh milioni 160.

“Kwa hili nasema siko tayari kuvumilia, nitafanya kazi na wale ambao tutaendana nao katika kuwatumikia wananchi.

“Wale watakaoona hawana sababu ya kuwatumikia wananchi, waondoke iwe ni kwa kuandika barua za kuacha kazi wenyewe au kwa namna yoyote watakayoona inawafaa,” alisema Kambona.

Katika hatua nyingine, mkurugenzi huyo amelazimika kuweka makazi yake kwa muda katika vijiji vya Sunya na Kijungu ili kusimamia kwa ukaribu miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa manne na vyoo katika Shule ya Sekondari Kijungi, vyoo na nyumba moja ya mwalimu iliyoko katika Kijiji cha Sunya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles