23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wakurugenzi watatu mikononi mwa JPM  

Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam*105 wengine wasubiri huruma yake

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAKURUGENZI zaidi ya 108 wa halmashauri mbalimbali nchini wanaweza kufikwa na uamuzi wowote  mbaya dhidi yao endapo Rais John Magufuli ataamua kufanyia kazi kwa vitendo Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2014/15.

Kusalimika au kutosalimika kwa wakurugenzi hao kunatokana na si tu hulka ambayo Rais Magufuli ameionyesha ya kutovumilia watumishi wasio waadilifu bali pia eneo hilo linalogusa halmashauri akihusika nalo moja kwa moja.

Wakati akitangaza baraza lake la Mawaziri, Rais Magufuli aliihamisha Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu  kwenda Ofisi ya Rais.

Kimsingi Wizara hiyo pamoja na mambo mengine inashughulika na masuala yote yanayohusu halmashauri na inasemekana hata uamuzi wa Rais Magufuli kuihamishia Wizara hiyo ofisini kwake kulitokana na dhamira yake ya kutaka kukomesha vitendo vya kifisadi kama vile vilivyojitokeza tena katika ripoti ya CAG.

Kutokana na ripoti ya sasa ya CAG ni wazi wakurugenzi wa halmashauri tatu zilizopata hati chafu wanasubiri uamuzi wa Rais Dk. Magufuli, kuhusu hatima ya vibarua vyao.

Mbali na hao pia wakurugenzi 105, wanangojea huruma ya kiongozi huyo hasa baada ya halmashauri zao kupata hati yenye mashaka.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG, Profesa Mussa Assad, aliyoikabidhi Aprili 25, mwaka huu kwa wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na ile ya Serikali za Mitaa (LAAC) ilizitaja halmashauri tatu zilizopata hati chafu kuwa ni Karatu, Hai na Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Halmashauri ya Mji wa Tunduma imepata hati mbaya ambapo watendaji wake wanadaiwa kuficha vitabu 79 vya mapato pamoja na hati za malipo zenye thamani ya Sh 178,511,580.

Mbali na hilo pia CAG alieleza kuwa halmashauri hiyo ya mji iliandaa malipo ya Sh 17,158,500 ambayo hayakuwa na viambatanisho pamoja na kutoandaa vitabu vya hesabu.

Halmashauri 105 zenye hati za mashaka

CAG Assad, alieleza kuwa pamoja na hali hiyo ukaguzi wake umebaini halmashauri 105 zimepata hati zenye mashaka ambazo ni Meru, Kongwa na Bukoba.

Zingine ni Kilwa, Ngorongoro, Mpwapwa, Muleba, Lindi, Kisarawe, Dodoma, Karagwe, Liwale na Mafia.

Katika orodha hiyo ipo pia Iringa, Kyerwa, Nachingwea, Mkuranga, Kilolo, Kibondo, Ruangwa, Rufiji/Utete, Ludewa, Kigoma, Babati, Ilala pamoja na Njombe.

Nyingine ni Moshi, Hanang’, Chamwino, Njombe TC, Mwanga, Babati TC, Kondoa, Makete, Rombo, Serengeti, Bahi, Biharamulo, Same na Musoma.

Pia ipo Rorya, Ngara, Magu, Bunda, Tarime, Misenyi, Misungwi, Musoma, Mbeya, Ulanga, Ukerewe, Mpanda TC, Rungwe, Morogoro, Geita TC, Mpanda, Chunya, Mvomero, Geita DC, Tunduru, Jiji la Mbeya, Masasi Mji, Bukombe, Songea, Mbozi, Masasi DC, Chato, Nyasa, Ileje, Mtwara DC, Sumbawanga DC na Shinyanga.

CAG Assad, pia amezitaja halmashauri za Mbarali, Newala, Nkasi, Shinyanga MC, Momba DC, Tandahimba DC, Manispaa ya Sumbawanga, Kishapu DC, Meatu DC, Nanyumbu, Korogwe, Maswa, Bariadi, Mtwara, Korogwe, Nzega, Manyoni, Mkinga, Kilindi, Sikonge, Singida, Lushoto, Igunga, Tabora, Pangani, Muheza, Urambo, Tabora, Jiji la Tanga, Handeni na Karatu.

Baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hizo za CAG, hivi sasa kamati za kisekta hasa zile za Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Serikali za Mitaa (LAAC), zimeanza kuchambua ripoti hizo ambapo baadaye zitawasilishwa bungeni na kujadiliwa kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, alitangaza bungeni kwamba halmashauri ambazo zitashindwa kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 zitafutwa kwa mujibu wa sheria.

Tayari Rais Magufuli, ameanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ya CAG ikiwemo kuwachukulia hatua watendaji waliotajwa na ripoti hiyo.

Siku moja baada ta ripoti hiyo ya CAG, Rais Magufuli, alitangaza kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba, kutokana na kutosimamia ipasavyo mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS) na kuisababishia nchi hasara ya mapato ya Sh bilioni 4 kwa mwaka.

Katika ripoti hiyo ya mwaka 2014/15 iliyoishia Juni 30, mwaka jana, Profesa Mussa Assad, alibaini madudu yakiutawala kila kona.

Ripoti hiyo imezimulika kwa kuzikagua taasisi za Serikali Kuu 199, Mamlaka ya Serikali za Mitaa 164 na Mashirika ya Umma 102 kati ya mashirika 186.

CAG Profesa Assad, alisema kwa upande wa miradi ya maendeleo ametoa ripoti 799 na kufanya jumla ya ukaguzi wa fedha.

Akisoma muhtasari wa ripoti kwa zaidi ya saa mbili, CAG Assad, alisema halmashauri zilizopata hati safi 47, hati zenye shaka 113, hati isiyoridhisha tatu na hati mbaya moja.

Kwa upande wa Serikali Kuu Wizara zilizopata hati safi ni 180, hati yenye shaka 18, hati isiyoridhisha moja na hakuna hati mbaya.

Huku kwa upande wa mashirika ya umma yaliyopata hati safi 99, hati yenye shaka matatu hakuna iliyopata hati isiyoridhisha wala hati mbaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles