Wakurugenzi Tanzanite One kortini kwa uhujumu uchumi

0
1362

Na JULIETH PETER

MANYARA

WAKURUGENZI wa mgodi wa Tanzanite One ulioko wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, wamefikishwa mahakamani kwa kosa uhujumu uchumi na kusababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 3.5.

Washtakiwa walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara, Simon Kobelo.

 Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Tarsila Asenga,  aliwataja  washtakiwa kuwa ni Hussein Gonga, Faisali Shabai, Abubakari Lombe na Anthony Maswi.

Asenga alidai washtakiwa wanadaiwa kuisababishaia Serikali hasara ya Sh 3,558,086,418.80 kwa kufanya makosa saba ya kuongoza genge la uhalifu, kushindwa kufuata amri halali za mkaguzi wa madini na kukaidi amri halali.

Makosa mengine ni kushindwa kufuata kanuni za usalama za madini, kukwepa kodi, kusababishia hasara mamlaka za Serikali na utakatishaji fedha.

Ilidaiwa kuwa watuhumiwa walimwaga maji ndani ya mgodi wa CFT uliokuwa ndani ya Tanzanite One ili kuzuia  wachimbaji kuchimba.

Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakma hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa sasa hadi jalada hilo litakaporudi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kutokana na hali hiyo, wamepelekwa rumande  baada ya hadi Juni 22 itakapotajwa tena.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here