25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wakurugenzi kukutanishwa kujieleza walichowafanyia wananchi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

SERIKALI kupitia Idara ya Habari Maelezo imeandaa mpango wa kuwakutanisha wakurugenzi na wakuu mikoa kuelezea kwa wananchi miradi iliyotekelezwa katika maeneo yao kwa fedha za Serikali.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi wakati wa mkutano na wahariri vyombo vya habari na waandishi jana Oktoba 29, 2023 kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), jijini Dar es Salaam.

Matinyi amesema wananchi wengi hawafahamu miradi inayotekelezwa katika mikoa yao, hivyo ni muda muafaka wa kujulishwa na viongozi wao wa mikoa na wilaya kile ambacho Serikali imekifanya.

Ameeleza kuwa programu hiyo itazinduliwa Jijini Dodoma Novemba 1,2023, November 2 tutakuwa Morogoro, November 3 Pwani na November 4 Dar es Salaam.

“Katika programu hii tutakuwa tunafika kwenye mkoa tutamwita mkuu wa mkoa na wakuu wake wa wilaya wataelezea, lakini pia tunataka kuwapa nafasi wakurugenzi ili kusikia habari za utekelezaji wa miradi ya Serikali,” amesema.

Katika hatua nyingine amesema Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye atakutana na wadau wahabari kujadili uundwaji wa kanuni za sheria ya habari ya mwaka 2016 ndani mwezi ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles