24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wakurugenzi Kagera watakiwa kuwawezesha maofisa ugani

Renatha Kipaka, Bukoba

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya mkoani Kagera wametakiwa kuwawezesha gharama za mafuta maofisa ugani ngazi ya kata ili waweze kufikia wananchi na kutoa huduma kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge wakati akipokea pikipiki 12 kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mbuge amesema mkoa huo unategemea mafanikio makubwa ya huduma zitakaofanywa na maofisa ugani kwenye maeneo ya wananchi.

“Wizaraiumetoa pikipkipi ikilenga kuongeza tija na ufanisi kwa kuhudumia na kuwafikia wananchi kusikiliza matatizo yao,” amesema Mbuge.

Amesema mkoa huo una ranchi za mifugo tano zilizopo wilaya za Missenyi, Karagwe na Muleba ambapo kuna maofisa ugani 146 wanohudumia sekta hiyo.

“Tunazo ranchi tano na bado nyingine zipo kwenye taratibu za kuanzishwa hiyo ni kupanua maeneo ya uwekezaji katika mifugo, sasa nyie wakurugenzi toeni mafuta watu wafanye kazi ikiwezekana ongezeeni pikipiki,”amesema Mbuge.

Ofisa Mifugo mkoani Kagera, Colman John, kumekuwa na tatizo la utendaji kazi usio ridhisha kwa maofisa ugani ngazi ya kata kwa kutokuwa na usafiri wa kufikia maeneo ya wafugaji.

Aidha, ujio wa pikipkipi hizo utasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuongeza tija inayotegemewa na Serikali katika kuboresha kazi zao.

John amesema mkoa unaidadi ya Ng’ombe 7,50,000 zilizo katika ranchi ya Taifa na katika makazi ya wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles