23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wakurugenzi halmashauri nne watumbuliwa majipu

simbachaweneNa Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

WAZIRI wa NChi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi),George Simbachawene amewasimamisha kazi wakurugenzi wanne wa halmashauri mbalimbali nchini.

Amechukua hatua hiyo baada ya wakurugenzi hao kubainika kutoa rushwa kwa wakaguziwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)   wapewe hati safi kuficha udhaifu katika hesabu zao.

Majina ya wakurugenzi na halmashauri zao kwenye mabano ni Ally Kisenge(Nanyumbu), Abdallah Mfaume(Mbogwe)na mwingine wa Kilolo ambaye hakumtaja jina lake.

Simbachawene amemvua madaraka Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tunduma,Halima Mpita, akidaiwa   kutumia vibaya madaraka yake.

Waziri aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa Kitundu anatuhumiwa kumwagiza Mweka Hazina, Majaliwa Byekwaso  kutoa Sh milioni tatu kwa wakaguzi   halmashauri hiyo ipewe hati safi.

“Kitendo cha kutoa fedha hizo ni kuwashawishi wakaguzi kuficha ukweli na kuandika hati safi wakati ndani
kuna uchafu.

“Hatuwezi kuwavumilia watendaji kama hawa kwa sababu wanarudisha nyuma maendeleo ya wananchi… tutawashughulikia
kwa mujibu wa sheria,”alisema Simbachawene.

Maofisa wa CAG waliopewa
fedha hizo ni  Stephen Uwawa,John Elias na Kilembi Nkole ili wabadilishe ripoti hiyo na kuficha uchafu
waliouona.

Alisema katika Halmashauri ya Nanyumbu, Juni mwaka
jana, Mkurugenzi Mohamed Kasenge alishirikiana na Mweka
Hazina, Pascal Malowe na Mhasibu,  Emanuel Muyigi  kutoa
rushwa ya  Sh milioni 3.5 kwa mMkaguzi F.Mwampashi ambaye
alipokea fedha hizo kwa niaba ya wenzake.

Alisema katika Halmashauri ya Mbogwe,Novemba mwaka jana,
Mkurugenzi Mfaume na Mweka Hazina, Lucas Ndombele walitoa
rushwa ya Sh milioni 16  kwa wakaguzi wanne ambao ni Mustapha Said,A. Kichanja,D. Mrima na A. Moha ili kuficha udhaifu waliouona.

Alisema katika halmashauri hiyo hiyo pia ilibainika matumizi
ya Sh milioni 236.8 yalifanywa bila ya kuwapo   nyaraka
zozote na Sh 144.1 zililipwa kwa mkandarasi bila kazi
kufanywa wakati  watumishi 82 waliohamishwa kutoka kwenye
halmashauri hiyo walilipwa mishahara.

Katika kikao kilichofanyika Novemba 30 kati ya wakaguzi na
watendaji wa halmashauri hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo,Sebastian Nasoro aliambiwa na watendaji
kuwa waliagizwa na Mkurugenzi Mfaume kutoa Sh milioni 12 kwa
wakaguzi hao ili wapewe hati safi.

Aliwataja wakaguzi waliochukua fedha hizo kuwa ni Rejea
Mattaka, Abdallah Kisura,A.J Kishire, Mustapha Said na A.M
Chanja.

Simbachawene alisema Felician Shilendi, mfamasia wa wilaya  a na Calistus
Salim, mhasibu wa afya wa halmashauri hiyo walitoa Sh milioni tatu kwa AJ Kishire ambaye ni mkaguzi wa
Mkoa wa Geita kwa ajili ya kuficha ukaguzi wa   Sh milioni 90 ambazo zilitakiwa kununua dawa na vifaa tiba vya halmashauri hiyo.

Kati ya Agosti 20 na 23 mwaka jana  katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, ilibainika kuwa Mhasibu, Lapson Pila alitoa Sh 245,000  ili aandikiwe hati safi.

Kwa Tunduma, waziri alisema Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo anadaiwa kuwatumia watoto wake katika shughuli za halmashauri na kuwalipa posho kinyume na taratibu.

Halima pia anadaiwa kuikosesha serikali mapato kwa kutumia madaraka yake vibaya wakati yuko mpakani.

Waziri amemteua Betram Mapunda kukaimu nafasi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles