27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wakurugenzi acheni kubana fedha za Lishe-Prof.Shemdoe

Na Atley Kuni, Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha fedha zinazotengwa katika bajeti kwa ajili ya shughuli za afua za lishe zinatolewa ili kutokwamisha kazi hizo.

Akifungua kikao cha siku tatu leo Aprili 28, 2021 mjini Dodoma, Prof. Shemdoe amesema kila mwaka serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kushughulikia masuala ya afua za Lishe, lakini tatizo hutokea wakati wa upangaji wa vipaumbele.

Amesema licha ya ongezeko la bajeti katika mamlaka za serikali za mitaa kutoka Sh. bilioni 11.6 mwaka 2017/18 hadi Sh bilioni 16.87 2019/20 lakini kumekuwa na utoaji wa fedha za afua za lishe usio wa kuridhisha.

“Kuanzia sasa pamoja na vipimo vingine vya ufanisi vinavyotumika kuwapima Wakurugenzi, suala la afua za lishe kitakuwa ni kigezo muhimu katika kuwapima watendaji hao, hivyo lazima wahakikishe masula yote ya suala la Lishe yanapewa kipaumbele” amesema Prof. Shemdoe.

Pia, Katibu Mkuu amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuzingatia miongozo inayotaka kutengwa Sh.1000 kwa kila mtoto aliye chini ya miaka mitano kwa ajili ya lishe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles