23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima watakiwa kutumia teknolojia bunifu za Veta kuongeza tija

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Dodoma

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imewaasa wakulima kutumia teknolojia zilizobuniwa na vyuo hivyo ili kuongeza tija kwenye kilimo.

Miongoni mwa teknolojia hizo ni mashine ya kutengeneza udongo kwa ajili ya kuotesha mazao ya bustani ambapo udongo wa kuoteshea ulikuwa ukitoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ikilinganishwa na mashine iliyopo Veta ya gharama nafuu.

Akizungumza Agosti 4,2024 kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema wanafunzi kwa kushirikiana na wanataaluma wa vyuo hivyo wamekuwa wakibuni teknolojia mbalimbali zinazowarahishia wakulima kulima kilimo chenye tija.

“Veta imegusa fani katika kila chuo kuendana na mazingira yake lengo ikiwa ni kufanya mhitimu kutafuta soko lake bila kukabiliwa na changamoto.

“Katika maonesho haya tunaonesha teknolojia ambazo zitafanya kilimo kukua kutokana na kupata mashine za gharama nafuu,” amesema Kasore.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, vyuo 80 vya Veta vimeshajengwa katika mikoa na wilaya na kwamba vyuo vipya 65 vinajengwa katika wilaya ili kuhakikisha kila wilaya inakuwa na chuo cha ufundi stadi.

Amesema vijana na wananchi watumie fursa ya uwepo wa vyuo hivyo ili kupata ujuzi na kuweza kujiajiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles