30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima waliolipwa fedha za korosho waipongeza serikali kwa usimamizi mzuri

Nora Damian, Tunduru

Baadhi ya wakulima wa korosho waliolipwa fedha zao katika Kijiji cha Mchopa kilichopo wilayani Tunduru, wameipongeza Serikali kwa usimamizi mzuri wa malipo ambao umewaongezea imani ya kuzalisha zaidi.

Hadi sasa katika Wilaya ya Tunduru wakulima 534 wamelipwa Sh milioni 550.7.

Mmoja wa wakulima hao, Issa Msanjo (48), ambaye katika msimu wa mwaka huu alipata kilo 1,600 amesema leo Novemba 20, kuwa ataongeza juhudi kwenye uzalishaji ili apate mazao mengi zaidi.

Mkulima huyo ameonyesha furaha yake kwa kupiga magoti huku akiwashukuru Rais Dk. John Magufuli na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homela, ambaye amefika kijijini hapo kuangalia utekelezwaji wa malipo hayo.

“Nimelipwa fedha zangu zote na sijakatwa chochote, namshukuru sana Rais Magufuli kwa hiki alichotufanyia sisi wakulima, ikiwezekana aendelee milele,” amesema Msanjo huku akiwa amepiga magoti.

Mkulima mwingine Ester Mchopa (58), amesema ana shamba la heka 10 lakini mwaka huu alilima heka moja iliyomwezesha kuvuna kilo 57.

“Kwa hamasa tuliyoipata mwaka huu nitakwenda kufufua heka nyingine moja,” amesema Mchopa.

Naye Shaibu Said, ambaye alipata kilo 405 amesema kwa sasa wakulima hawana hofu tena kwani wana uhakika wa soko.

Hata hivyo, wakulima hao wameiomba serikali kuangalia upya gharama za pembejeo hasa dawa (sulphur) ambayo ni muhimu katika kilimo cha korosho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles