21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

WAKULIMA WA UFUTA LINDI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA

Hadija Omari, Lindi

Wakulima wa zao la ufuta mkoani Lindi, wametakiwa kuzingatia ubora wa zao hilo ili kuwavutia wanunuzi na kuendelea kupata bei nzuri.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi, Robert Nsunza alipokuwa akizungumza wakati wa mnada wa ufuta mkoani humo.

Nsunza amesema ili kuendelea kupata bei nzuri ni vyema kwa wakulima wa zao hilo kuzingatia ubora katika uandaaji.

“Sisi sote ni mashaidi huu ni mnada wa  tatu kufanyika lakini kila mnada tunashuudia bei zikiwa zinapanda hii ina maana kuwa wanunuzi wameona ubora wa ufuta wetu,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Amcos Lindi, kinachounganisha wanachama na wakulima wa Halmashauri za kilwa , manispaa ya  Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Rashidi Masoudy ameishukuru serikali ya Mkoa kwa kutengeneza mfumo mpya wa ununuzi wa zao hilo kwani umeanza kuleta tija kwa wakulima wao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles