26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Wakulima wa parachichi nchini washauriwa kuongeza uzalishaji

Na Safina Sarwatt, Arusha

Wakulima wa Parachichi nchini wameshauriwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo, kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa katika soko la kitaifa na kimataifa.

Mkurugenzi Mtendaji Avomeru Group, Jasse Oljange ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, katika ziara ya mafunzo ya kwa waandishi wa Hhabari kutoka Kanda ya Kaskazini iliyoratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (COSTECH).

Amesema uhitaji wa zao la parachichi ni kubwa kwenye soko la dunia na viwanda vya ndani hivyo wafanyabiashara na wakulima ni vema wawekeze na kuzalisha kwa wingi katika zao hilo ili kukidhi mahitaji.

Amesema parachichi aina HASS ndiyo inayohitajika zaidi kwenye viwanda, kwa ajili yakutegenezea vipodozi na mafuta ya kupikia.

“Ni vyema sasa wakulima wadogo na wa kati kuweza kuona fursa hii na kuongeza uzalishaji pamoja na kutambua jamii ya parachichi yanayohitajika katika soko la kimataifa hasa parachichi jamii ya HASS, lakini jamii ya FUERTE na parachichi ya asilia yamekuwa kati ya parachichi yenye soko kubwa,”amesema Oljange.

Utafiti unaonyesha kuwa soko kubwa la bidhaa hiyo linapatikana katika mataifa mengi ya Ulaya, kwani Bara hilo linanunua zaidi ya tani milioni moja ya parachichi kwa mwaka na taasisi inayojihusisha na zao hilo duniani (WAO) imekadiria kuongezeka kwa uhitaji kwa asilimia 50 zaidi katika miaka kumi ijayo.

Aidha, amesema mataifa ya Ufaransa, Uingereza na Uholanzi ni kati ya mataifa yanayonunua zaidi bidhaa hizi kutoka Tanzania.

Kwa takwimu za mwaka 2018, bara la Ulaya pekee lilichukua asilimia 85 ya soko la parachichi kutoka Tanzania ambayo ni mzalishaji mkubwa wa pili nchi za Afrika wa zao hilo ikifuatiwa na nchi jirani ya Kenya, ambayo inazalishaji wa tani 190,000 kwa mwaka.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania imekuwa na kipaumbele katika kutafuta masoko kwa ajili ya wakulima wa bidhaa hizo.

Wizara ya Kilimo imekuwa kupaumbele katika kutafuta fursa ya kuweza kusafirisha bidhaa ya maparachichi katika soko la China kwani soko hili linanunua bidhaa za fedha za Kimarekani zaida ya dola milioni 108 kwa mwaka hii ikiwa inaonyesha ni soko la uhakika kwa wakulima wa Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles