24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wa korosho Lindi wajengewa kituo cha malipo

 HADIJA OMARY-LINDI

HATIMAYE ucheleweshwaji wa Fedha za malipo ya wakulima wa Wilaya ya Liwale wanaohudumiwa na chama kikuu cha Ushirika Runali kinachojimuisha wakulima wa Wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea mkoani Lindi, itabaki historia baada ya chama hiko kujenga kituo cha malipo kitakachotumika kuandaa na kuhakiki malipo ya wakulima hao kwa haraka zaidi

Kituo hiko cha malipo kimejengwa katika Kata ya Nangando Wilayani Liwale ambapo kimewekwa jiwe la msingi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kuudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Serikali Wilayani humo pamoja na viongozi wa vyama vya Msingi, Amcos za wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale yenyewe.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Chama kikuu cha Ushirika Runali, Jahida Hasani alisema kuwa ujenzi huo wa kituo cha malipo mpaka kukamilika kwake utagharimu Sh milioni 65 na kwamba kitaanza kutumiwa na viongozi hao katika msimu huu wa korosho wa 2020/2021

Hata hivyo, meneja huyo alieleza kuwa lengo kubwa la kujenga kituo hiko ni kuwaleta pamoja viongozi na watendaji wa vyama vya msingi na kuandaa malipo ya wakulima jambo ambalo apo awali ilikuwa ni changamoto.

“Kwenye eneo hili la ujenzi wa kituo cha malipo unaenda sambamba na ujenzi wa ghala dogo ambalo litakuwa likitumika kuhifadhia pembejeo pamoja na vifungashio jambo ambalo nalo ilikuwa ni changamoto kwetu kwani tulikuwa tunalazimika kukodi maghara kwa ajili ya kuhifadhia vitu hivyo,” alifafanua.

Akizungumza na viongozi hao, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi mara baada ya kukagua jingo hilo na kuweka jiwe la msingi alikipongeza chama hiko kwa namna kinavyoendelea kutoa huduma bora kwa wananchama wake kwa kuzikabili changamoto wanazokutana nazo.

Pamoja na pongezi hizo Zambi pia aliutaka uongozi wa Bodi wa chama hicho cha Runali kujenga kituo kingine cha malipo katika Wilaya ya Ruangwa ili changamoto hiyo ya ucheleweshaji wa malipo iwe Historia sio tu kwa wakulima wa Liwale bali kwa wananchama wote wanaohudumiwa na chama hiko

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles