27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wa kawaha walia bei kuwa ndogo

Upendo Mosha, Arusha

WAKULIMA wa kahawa nchini wamelalamikia kupata hasara kila msimu wa mauzo kutokana na bei ndogo wanayoipata, jambo ambalo haliendani na gharama halisi za uzalishaji wa kahawa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana katika shamba darasa la Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Nchini (TaCRI), lililopo katika maonyesho ya wakulima ya nanenane Kanda ya kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya Themi Arusha, baadhi ya wakulima hao walisema bei ya zao hilo inazidi kuwadidimiza wakulima.

Philemoni Matai, mkulima wa kahawa wa Kijiji Cha Masama Mula, alisema wamekuwa wakipata hasara ambapo gharama za uzalishaji wa kahawa kwa kilo moja ni Sh 4,500 huku Bei wanayoipata sokoni kiwa ni Sh 3,900.

“Tunapata hasara ya mamilioni ya shilingi kila mwaka wakati wa msimu wa kahawa bei inakuwa ni ndogo sana ikilinganishwa na gharama tunazotumia kuzalisha, kilimo hiki kinakatisha tamaa, ni muhimu Serikali kuangalia suala hili,”alisema.

Alisema mbali na changamoto ya bei ya zao hilo kuwa chini, wanakabiliwa na ukosefu wa pembejeo jambo ambalo limekuwa likisababisha kuongeza gharama katika uzalishaji.

Naye Isaria Swai, mkulima wa kahawa kutoka Kijiji Cha Bweera, alisema licha ya kupatiwa mbegu bora za kahawa kutoka TaCRI, suala la pembejeo ni changamoto na kwamba ni vema Serikali ikaona jinsi kuboresha kilimo hicho ikiwemo kuweka mfumo rafiki wa upatikanaji wa pembejeo.

“Tunapatiwa mbegu bora kutoka TaCRI ambazo zinakinzana na magonjwa, lakini bado kunachangamoto ya wadudu wadogo wadogo, ni wakati wa Serikali kuangalia zao hili ili liwatoe wakulima zaidi,”alisema.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka TaCRI, Sophia Malinga, amekiri kuwepo kwa changamoto nyingi zinazo wakabili wakulima ikiwemo ukosefu wa maji ya kutosha ya umwagiliaji wa bustani za miche katika halmashauri zote nchini.

Akizungumzia suala la bei ya kahawa, Meneja wa Mauzo na Ubora kutoka Bodi ya Kahawa nchini (TCB), Frank Nyarusu, alisema msimu kwa sasa wameruhusu wanunuzi binafsi kununua kahawa kwa wakulima kupitia  vyama vya ushirika jambo ambalo litasaidia kuondoa ukandamizaji kwa wakulima.

“Msimu wa kahawa umeshaanza na karibu asilimia 30 ya kahawa imekwisha kukusanywa na sasa unapelekwa kwenye viwanda na baadhi ya mauzo yameanza kufanyika, tunategemea bei ya kahawa utaendelea kuwa nzuri katika soko la dunia licha ya changamoto ya Corona”alisema

Aidha alisema katika msimu wa 2019/2020 walifanikiwa kukusanywa tani elfu 59 katika msimu 2020/2021 wamelenga kukusanywa zaidi ya tani 70.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles