29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Wakulima nchini wampongeza Rais Samia kwa kufanya mageuzi kwenye Kilimo

Ramadhan Hassan, Dodoma

WAKULIMA wameomba kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan ili wamweleze changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo huku wakimpongeza kwa mageuzi makubwa ambayo ameyafanya katika sektaya kilimo.

Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni mkulima, Mariamu Ditopile.

Ombi hilo limetolewa leo Agosti 21,2022 jijini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni mkulima, Mariamu Ditopile wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Mariam amesema wanatambua kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia hivyo wanaomba kukutana nae ili wamweleze changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo.

“Sisi tunatambua kazi nzuri ambayo anafanya na kwa hili tunasema asante mheshimiwa Rais sisi tupo pamoja na wewe kwenye kila ambacho unafanya,”amesema Mbunge huyo.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ambapo kwa mara ya kwanza bajeti ya uzalishaji wa mbegu imeongezeka kutoka Sh bilioni 10.5 hadi Sh bilioni 43.03.

Amesema Rais Samia ndani ya muda mfupi amewezesha kupatikana kwa bajeti bora ya kilimo ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2022/23, Wizara ya Kilimo imetengewa Sh bilioni 751 huku Sh bilioni 631 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Mariam ameongeza kuwa ongezeko la bajeti ya kilimo kwa mwaka huu wa fedha ni takribani asilimia 300 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2020/21 ambapo kiasi kilichotengwa ni Sh bilioni 229 na kati ya fedha hizo ni Sh bilioni 150 pekee ndio zilienda kwenye miradi ya maendeleo.

“Rais Samia pia amejidhatiti kwenye eneo la tafiti za Kilimo, Bajeti ya tafiti za Kilimo imepanda kutoka Sh bilioni 7.3 kwa mwaka 2020/21 hadi Sh bilioni 40 kwa mwaka huu wa fedha. Tunamshukuru Rais pia kwa kupandisha bajeti ya Uzalishaji mbegu kutoka Sh bilioni 5.4 hadi Sh bilioni 43 kwa mwaka huu wa fedha 2022/23,” amesema Mariam.

Amesema pia wameshuhudia utaratibu mzuri wa kuwawezesha wakulima nchini kupata Mbegu za alizeti ambapo gharama zote ni Sh 3,500 tofauti na bei ambayo haikuwa na ruzuku ambayo ilikua ni Sh 7,000 hadi 8,000.

Amebainishwa kuwa kwa namna ambavyo Rais Samia ameonesha mageuzi makubwa kwenye sekta ya kilimo wao kama wakulima wanampongeza kwa jitihada za dhati za kuwakomboa kwani ni wazi mchango wa mbolea ni mkubwa katika sekta ya kilimo hususan katika kuongeza tija.

“Tunamshukuru Rais Samia na Serikali yake kwa usikivu wao kwetu sisi wakulima kwa kutuletea mfumo mzuri wa mbolea ya Ruzuku pamoja na kutoa kipaumbele kwa wazalishaji wa ndani ili kulinda viwanda vyetu, ajira na Usalama wa chakula,”amesema Mariam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles