26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA MBULU WAHAMASIKA KULIMA PARETO

Na ELIYA MBONEA-MANYARA



BAADHI ya wakulima wa Kata ya Tumati na maeneo ya Mamaisara wilayani Mbulu mkoani Manyara, wameonyesha nia ya kuanza kulima zao la biashara la pareto kwa wingi, baada ya kuhakikishiwa soko la uhakika.

Wakulima hao wakizungumzia kuhusu nia ya kurejea kulima zao hilo hivi karibuni wilayani humo, walisema waliamua kuachana na kilimo hicho kutokana na kutoona faida yake hasa katika soko.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake, Mkazi wa Kata ya Tumati, Zacharia Boay, alisema uhamasishaji uliofanywa umewapa ari mpya ya kurejea kulima zao hilo la kibiashara.

“Wakulima wengi eneo hili kwa hakika wamekuwa na hamasa kubwa ya kuanza kulima tena zao la pareto, baada ya viongozi wa halmashauri kuwahakikishia uwepo wa soko la uhakika tofauti na awali,” alisema Boay.

Mkulima huyo aliwataka wakulima wenzake katika maeneo hayo kuhakikisha wanaitumia fursa hiyo ya kilimo cha pareto kujiongezea kipato badala ya kuendelea kulima mazao ya chakula pekee.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, alisema Serikali wilayani humo itahakikisha inawasaidia wakulima kufikia malengo yao ili wapate faida iliyopo kwenye kilimo.

“Tumejipanga kuhakikisha wataalamu wa zao la pareto wanawezeshwa ili wawasaidie wakulima kufikia malengo yao ya kuvuna mazao mengi na yenye tija.

“Pareto inayozalishwa kwenye maeneo ya Wiyala yetu ya Mbulu, ni bora kabisa duniani ikiwa inazidiwa tu na pareto inayozalishwa nchini Australia,” alisema Kamoga.

Mbali na kuwahimiza wakulima wilayani humo kulima zao hilo, Kamoga aliwataka pia wawekezaji kutoka nje ya wilaya kwenda kuwekeza katika kilimo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles