22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima Kagera waomba kujengewa ujuzi ili kuongeza uzalishaji

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Baadhi ya wakulima mkoani Kagera wameiomba Serikali kuwajengea ujuzi katika kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha ili kujipatia kipato zaidi.

Wakulima hao wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Mtanzania Digital iliyofika kwenye maonyesho ya wakulima NaneNane yanayofanyika eneo la Kyakailabwa kata Nyanga Manispaa ya Bukoba mkoani humo.

Mchakataji wa zao la karanga mkazi wa Wilaya ya Misenyi, Twaha Salim amesema asilimia kubwa ya wananchi ni wakulima lakini hawana ujuzi wa kuongeza thamani ya mazao.

Amesema endapo serikali itaweka nguvu kubwa katika elimu ya ujuzi wa kuongeza thamani ya mazao wayapata kipato zaidi.

“Watu wengi wamechukia kilimo lakini njia ya kuongeza thamani itawarejesha kwenye sekta hii muhimu kwani faida kubwa itapatikana kwenye kilimo akifika sokoni,”amesema Salimu na kuongeza kuwa:
“Mfano mimi ninaongeza thamani kwenye zao la karanga naingia sokoni kununua debe la karangara za maganda kwa Sh 10,000 nazibangua ninatoa kilo nne safi nauza kwa Sh 3,500 kwa kilo napata Sh 1,4000 hadi Sh 16,000,”amesema Salimu.

Upande wake msindikaji wa nafaka za lishe wilayani Karagwe, Malselina Kweyamba amesema licha ya kutengeneza lishe ya nafaka na kuiongeza thamani bado napata fida zaidi.

Kweyamba amesema amekuwa akilima mahindi, karanga na viazi lishe na kuviingiza sokoni lakini faida haionekani.

Amesema hali hiyo ilimkatisha tamaa na kuamua kutafuta ujuzi kwa kuongeza thamani ndipo aliongeza bidii ya uzalishaji.

“Ukilima ekari moja kwa kufuata kanuni unavuna kwa tija lakini ukiongeza thamani unajitafutia faida zaidi lengo letu tuingie uchumi wa familia na nchi pia,”amesema Kweyamba.

Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Kagera, Loose Baraka amesema mkoa una zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanategemea kipato chao kutoka kwenye kilimo.

Baraka amesema mchango wa kilimo kwa maana ya mkoa ni mkubwa kwa mazao yanayolimwa ni kahawa, ndizi, maharage na mikunde.

“Huko kote kuna mzunguko wa fedha na hata ikapewa umuhimu wa maonyesho ya Nane Nane na kuona michango yake kwenye sekta hiyo,”amesema Baraka.

Kwa msimu uliopita mkoa ulizalisha zaidi ya tani milioni tatu kwenye mazao ya mizizi, nafaka na mikunde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles