25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima 2,000 wanufaika na mbegu za kisasa

Mwandishi Wetu -Dodoma

MRADI wa kuendeleza zao la mtama nchini wa kampuni ya Bia ya TBL Plc, unaendelea kunufaisha wakulima wa zao hilo mkoani Dodoma, ambapo wanapatiwa mbegu za kisasa, mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa kinachofanikisha kuongezeka kwa mavuno pia wanakuwa na uhakika wa kuuza mavuno yao kwa kampuni hiyo.

Akizungumza n kwa niaba ya wakulima wenzake katika mahojiano yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, Issa Dinya,  alisema kutokana na mradi huo wameanza kulima zao la mtama kibiashara kwa kuwa wana uhakika wa soko tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walilima zao jilo kwa ajili ya matumizi ya chakula.

Kupitia mradi huo wa majaribio unaoendeshwa kwa ushirikiano wa TBL Plc, WFP na FtMAumenufaisha zaidi ya wakulima wadogo 2,000 ambao mavuno yao yaameongezeka kwa asilimia 77 na maisha yao kuwa bora, mkakati wa kampuni ni kuinua wakulima wadogo kupitia kununua mazao yao kwa bei nzuri kwa ajili ya malighafi za kuzalisha biadhaa zake.

Mradi huo wa ushirikiano ulianza mwezi Januari Mwaka 2020 ambapo TBL Plc, Ilikubaliana na wakulima kununua zao lao la mtama mkoani Dodoma na Manyara, ambapo taasisi za WFP na FtMA zimewezesha wakulima kupata mbegu za mtama, bima, ushauri wa kilimo cha kitaalamu na uhakika wa masoko.

Akizungumzia mafanikio ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Plc, Philip Redman, alisema anafurahia kuona mafanikio ya mradi huo wa mtama kwa kuwa umeenda sambamba na mkakati wa kampuni hiyo wa kuboresha kilimo cha mtama nchini Tanzania na kuwezesha wakulima wa zao hilo kuendelea kuwa na kipato cha uhakika kuanzia sasa na katika siku za mbele.

 “Mkakati wetu wa kununua malighafi ni mkakati wetu mojawapo wa kuchangia jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa nchi,” alisema Redman.

Akiongea katika moja ya mikutano ya uhamasishaji wa kilimo cha mtama mkoani Dodoma karibuni, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa, Mustapha Yusuf, aliipongeza TBL kwa mkakati wake wa kununua malighafi kutoka kwa wakulima nchini.

“Mkakati huu kwa kiasi kikubwa umeleta hamasa kwa wakulima kuzalisha zao la mtama kibiashara nchini na utawanufaisha kwa kuboresha maisha yao sambamba na kupata mbegu bora ambazo zinafanikisha kuzalisha mtama wenye kiwango kizuri na mavuno yao kuongezeka,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles