27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wakongwe kazini rithisheni ujuzi na utaalam kwa vijana wapya

Na Zuena Msuya Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja ametoa wito kwa watumishi wenye ujuzi na uzoefu wa muda mrefu sehemu za kazi kurithisha ujuzi walionao kwa watumishi wengine  ili kuendelea kutekeleza majukumu kwa ufanisi kwa manufaa ya nchi na Taifa kwa jumla.

Mhandisi Masanja alitoa wito huo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi ya Katibu Mkuu baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni, kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Said, ambae ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Aprili 27, 202, Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Said, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (kulia) na Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Nishati Mhandisi Leonard Masanja (Kushoto), wakisaini nyaraka kabla ya makabidhiano ya ofisi yamefanyika Aprili 27, 2021, Jijini Dodoma, wanaoshuhudia ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kheri Mahimbali (kushoto), na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa wizara hiyo, Anna Ngowi (katikati)

Makabidhiano hayo, pia yalishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kheri Mahimbali, Wakuu wa Vitengo na Idara pamoja na Menejimenti.

Katika makabidhiano hayo, Mhandisi Masanja alieleza kuwa katika utumishi wa umma kila siku watumishi wanastaafu wakiwa na ujuzi na uzoefu wao kazini licha ya wengine kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Hivyo basi, ni vyema wakongwe na wenye ujuzi na uzoefu kuhakikisha wanarithisha utaalamu na ujuzi wao kwa watumishi wengine ili kuendelea kutekeleza majukumu ya serikali ya kuwahudumia wananchi kwa ufasaha.

“Wakongwe sehemu za kazi, viongozi wa maeneo mbalimbali hakikisheni mnapoondoka katika nafasi hizo, mliowaacha wanawakumbuka kwa mlichokifanya, warithisheni mazuri mlionayo, tuache tabia ya kukumbatia ujuzi na uzoefu tulionayo na kuacha tabia ya ubinafsi,hii ni kwa faida ya vizazi vyetu vijavyo na Taifa kwa ujumla,” alisisitiza Mhandisi Masanja.

Vilevile aliwaonya baadhi ya viongozi wenye tabia ya kupendelea baadhi ya watumishi katika kugawa majukumu, na kujipendelea wao katika kupata maslahi kuwa kwa kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za utumishi wa umma na kwamba mwisho wake kuharibu kazi za serikali.

Masanja alisisiza kuwa tabia hiyo imekuwa ikijenga uadui katika sehemu za kazi, kuweka matabaka na hivyo kuzorotesha utendaji kazi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Said, aliwashukuru watumishi wa wizara ya nishati kwa ushirikiano waliouonyesha kwake wakati akiwa katibu Mkuu katika wizara hiyo.

Pia alitoa wito kwa viongozi na watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana, kuheshimiana kwa kuwa kufanya hivyo kunastawisha utendaji kazi na kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na kwa usahihi.

Vilevile alitaka viongozi kutumia lugha za staha na kauli nzuri kwa watumishi waliochini yao katika mazingira yote ya kazi,na pia kuwafanya kuwa sehemu ya familia ama rafiki zako kwakuwa muda mwingi wanakuwa wote na wategemeana.

“Usifanye kazi ili uonekane na mtu fulani huku ukiwanyanyasa wengine, unapaswa kutekeleza majukumu yako, uongozi ni dhamana yeyote anaweza kuwa, pia waliochini yako ndio wanaoweza kukujenga kama kiongozi au kukubomoa, ni vyema kufanya kazi na watu wote na kwa usawa,” alisema Mhandisi Zena.

Sambamba na hilo aliipongeza uongozi wa wizara ya nishati pamoja na watumishi wake kwa kazi nzuri zinazoendelea kufanyika za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika sekta ya nishati ikiwemo Umeme na Gasi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kheri Mahimbali, alimueleza Mhandisi Said kuwa, wataendelea kushirikiana na ofisi yake kule Zanzibar katika kuwahudumia wananchi katika sekta ya nishati.

Hata hivyo, Mahimbali alimueleza kuwa asisite kueleza changamaoto zozote zitazazokuwa zikiwakabali katika sekta hiyo kwa kuwa bara na visiwani ni nchi moja, na aendelee kuwa balozi mzuri katika kuiwakalisha Tanzania kwenye sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles