30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAKONGO WANAOINGIA NCHINI KUFUATILIWA AFYA ZAO

NA VERONICA ROMWALD– DAR ES SALAAM


SERIKALI imeweka utaratibu mpya wa kuwasajili katika fomu maalumu na kuwafuatilia hadi majumbani,  wasafiri wote wanaoingia nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema jana kuwa utaratibu huo mpya umelenga kufuatilia mwenendo wa hali zao za afya kutokana na mlipuko wa  ebola nchini humoi, ulioripotiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) Mei 21, mwaka huu.

Ummy alisema hadi sasa watu 43 wamegundulika kuugua na wanne wamefariki dunia.

“Wananchi wasiwe na hofu, ebola haipo nchini, tunafuatilia kwa karibu na tumeimarisha mifumo ya ukaguzi.

“Lakini wasafiri wanaotoka Kongo naomba wajue hatua hii haijalenga kuwabagua bali tunataka kulinda afya za Watanzania.

“Watapimwa joto lao la mwili na watasajiliwa  katika fomu maalumu itakayotuwezesha kuwafuatilia kwa karibu, kwa sababu mtu anaweza kupimwa mara ya kwanza asionyeshe dalili, tunataka kuchukua tahadhari,” alisema.

Waziri Ummy alisema   serikali imeagiza mashine nne za ukaguzi ambazo zitapelekwa   mipakani.

Alisema   timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI zipo Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya na Songwe kushirikiana na wenzao  o kwenye mikoa hiyo kupanga mikakati ya namna ya kudhibiti ugonjwa huo.

Binadamu huwa anapata virusi vya ebola kutoka kwa wanyama na   kuambukizana.

Hata hivyo,  hadi leo watafiti hawajui kabla ya mnyama kupata virusi hivyo huwa vinaishi katika mazingira yapi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles