24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wakimbizi 500 wa Burundi waugua kipindupidu

steven kebweNA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM
UGONJWA wa kipindupindu umelipuka katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo mkoani Kigoma ambako wakimbizi 558 kutoka Burundi wamekumbwa na ugonjwa huo.
Pamoja na kuibuka kipindupidu katika kambi hiyo, watu 15 walikuwa wamefariki dunia kufikia juzi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Steven Kebwe, alisema Aprili 24 mwaka huu, wakimbizi 2,458 walikuwa wakiharisha na kutapika katika kambi hiyo huku sampuli 11 kati ya 13 zilizochukuliwa juzi zilithibitisha kuwa wanaugua kipindupindu.
“Tumeshirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na tayari tumepeleka timu ya wataalamu ambao wametembelea maeneo ya Kagunga na Nyarugusu kutathmini na kutoa elimu ya afya kwa umma.
“Tumefanya tathmini katika mikoa ya Kagera, Geita na Katavi ambayo inapakana na Burundi,” alisema Dk. Kebwe.
Alisema zimepelekwa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya dharura pamoja na kuanzisha mfumo wa kufuatilia magonjwa yakiwamo ya mlipuko katika maeneo yaliyoathiriwa.
Kwa mujibu wa Dk. Kebwe, kipindupindu kinatokana na kula chakula au kunywa kinywaji chenye vimelea vinavyosababisha kuharisha ambavyo hupatikana kwenye kinyesi, matapishi au majimaji kutoka kwa mgonjwa.
Alizitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni kuharisha mfululizo bila maumivu ya tumbo, kinyesi cha majimaji kinachofanana na maji ya mchele, kutapika mfululizo, kuishiwa nguvu na ndani ya saa sita kama hakuna huduma mgonjwa anaweza kufa.
Kuhusu gharama za matibabu, alisema Serikali inatumia fedha kutoka kwenye mfuko wa akiba ya magonjwa ya dharura na mlipuko ambazo zitarejeshwa baadaye na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles