Wakili wa Mbasha augua, kesi yaahirishwa

0
1327
Emmanuel Mbasha
Emmanuel Mbasha
Emmanuel Mbasha
Emmanuel Mbasha

Veronica Romwald na Zainabu Abdillah (MUM), Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jana imeahirisha kesi ya ubakaji inayomkabili mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili, Emmanuel Mbasha hadi Septemba 19, mwaka huu kutokana na wakili anayemtetea, Mathew Kakamba, kuugua shinikizo la damu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwendesha Mashitaka wa Polisi na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai Mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya Kakamba kuieleza Mahakama kuwa hawezi kuendelea na shauri hilo kutokana na maradhi yanayomsumbua.

“Mshitakiwa alifika mahakamani kawaida na leo (jana) tulikuwa na mashahidi wawili, lakini kutokana na ombi la Kakamba kuiomba Mahakama kuahirisha kutokana na kuugua, Hakimu Williberforce Luwhago hakuwa na pingamizi ambapo aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 19, mwaka huu,” alidai Katuga.

Katika kesi hiyo, Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa injili, Flora Mbasha, anadaiwa kumbaka shemeji yake (17) kati ya Mei 23 na 25, mwaka huu eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here