24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wakili Marenga: Mambo haya yanakandamizi taaluma ya Habari

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Wadau wa Habari nchini wameendelea kuichambua Sheria ya Habari huku wakitaja vifungu vinavyolenga kuminya uhuru wa wanahabari.

Wakili James Marenga akizungumza Juni 10, 2022 Dar es Salaam katika hafla iliyokutanisha Wanahabari ikilenga kujadili mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari nchini yaliyowasilishwa serikalini.

Marenga amezitaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 ambayo inasimamia radio, TV na Mitandao ya Kijamii, Sheria ya Haki ya Kupata Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya makosa ya Mtandao ya 2015 zikiwemo kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2018 ziliyogawanywa katika vipengele mbalimbali.

Amesema katika sheria ya sasa ina vifungu vingi ambavyo vinaingilia uhuru wa wanahabari kutekeleza majukumu yao huku pia ikiwa hatoi kikomo cha adhabu iwapo mwandishi atatiwa hatiani.

“Kuna vifungu vingi ambavyo vinaleta ukakasi kwenye tasnia hii ya habari ambavyo tumependekeza viondolewe, mfano ukingalia vifungu vya 4(2), 5(2), 6(2), 7(1) (g), 7(2)(b), 7(3)(b), 8(2), 9(b), 10(2), 11(2), 12(2), 13(2),14(2)(a), 14(2)(b), 15(2), 16, 17(2), 18(2), 19(2), 20(2), 21(2), 22(1), 22(2), 23(2), 24 (2)(a), 24(2)(b), 26(3), 27, 29 na 45(3) hivi vimebebwa na neno “Not Less Than” likimaanisha ‘Si Chini Ya’ ambavyo kwa tafsri ya haraka vinaonekana kuwa ni changamoto.

“Mapungufu haya ya kutumia ‘not less than’ yanawapa mwanya kwa wale ambao wanatoa maamuzi kwa mfano mahakimu au majaji wakati mwingine kuweka adhabu kubwa zaidi kinyume na uhalisia wa kosa lilotendekaau adhabu zingine.

“Hivyo tunasema sheria inapaswa ioneshe ukomo wa adhabu, mfano badala ya kuandika ‘Less Than’ iwe ‘not more than’ (si zaidi ya) jambo ambalo tunaamini kuwa itatumika ili kutenda haki na usawa pale mwanahabari au chombo kinapoingia matatizoni,”amesema Wakili Marenga.

Wakili Marenga ameendelea kubainisha kuwa miongoni mwa vifungu vingine vyenye mapungufu katika sheria hiyo ni pamoja na 4 (1), 5 (1), 6(1),7(1), 7(3), 9, 11, 22(1) na 22(2) ambavyo vinazungukwa na neno “Intentionally” (kwa kudhamiria).

“Kuna umuhimu wa kurekebisha sheria na kufuta neno “kwa kudhamiria”. Haiwezekani kuthibitisha nia ya kufanya uhalifu kwa maneno ya kubahatisha,”amesema Marenga nakuongeza kuwa kuna maneno ambayo yanautata likiwamo “Chapisha”.

“Wakili Marenga amevitaja vifungu vingine kuwa ni kile cha 31 ambacho kinatoa mamlaka kwa polisi kutoa amri ya kumshinikiza mtu kutoa data zilizohifadhiwa kwenye kompyuta yake. Kifungu kingine ni cha 38 ambacho hiki kinataoa mamlaka ya kesi kuamuliwa bila mhusika (mlalamikiwa)kuwepo jambo ambalo ni hatari,” amesema Marenga.

Pia amezitaja baadhi ya nchi ambazo sheria zao ni rafiki kuwa ni Nigeria, Kenya, Ghana na nyingine.

Katika hatua nyingine Marenga amesema kuwa kunapaswa kuwapo na chombo cha wanahabari wenyewe kitakachosimamia tasnia hiyo kama ilivyo katika fani nyingine.

“Ikiwa mwanasheria anahukumiwa na wanataaluma wenzake kwenye bodi yao, mwanahabari naye anapaswa kuhukumiwa kwenye bodi itakayoundwa na wao wenyewe na si bodi iundwe na serikali ama waziri,” amesema Marenga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles