22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Wakili Madeleke ataka sheria ya uhujumu uchumi kurekebishwa

Na Brighiter Masaki
Dar es salaam.

Wakili wa kujitegemea wa Mahakama Kuu nchini Peter Madeleka, amesema Sheria ya makosa ya uhujumu uchumi,utakatishaji fedha,na mwenendo wa makosa ya jinai inamapungufu makubwa na imekuwa ikitekelezwa kunyume na bunge lilivyokusudia wakati wa kuzitunga.

Akizungumza mapema Leo jijini Dar es Salaam, Wakili Madeleka, anasema sheria hiyo kwa sasa imekuwa ikitumika vibaya kwa watu kuwekwa gerezani kwa muda mrefu kwa kigezo cha upelelezi haujakamilika lengo likiwa ni kuwakandamiza wanyonge ambao hawana uelewa wa sheria hizo.

“Sheria ya uhujumu uchumi kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikitumika vibaya na uhujumu uchimi na utakatishaji fedha inatumika kama nyundo ya kuwapiga wanyonge kuwaumiza na kwa bahati mbaya sana hawana uelewa wa namna sheria zinavyosema” amesema Wakili Madeleka
amesema kwa sasa ukishtakiwa kwa makosa hayo utakaa gerezani kwa muda usiopungua mwaka mmoja kwa kisingizio cha upelelezi kuto kukamilika ambapo jambo hilo ni kinyume na sheria.

“Napenda kuwafahamisha watanzania kifungu cha 21 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya uhujumu uchumi kinasema pamoja mambo mengine ili upelelezi wa makosa ya uhujumu uchumi uweze kufanyika lazima kuwepo amri na itangazwe kwenye gazeti la serikali’’ amesema
Wakili Madeleka amesema sharti hilo ni lazima na lisipotekelezwa manaake shauri nzima na mwenendo wake unakuwa batili hivyo mashauri yote ambayo yapo Mahakamani na upelelezi haujakamilika ni kwa sababu kanuni zimekiukwa.

“Hakuna gazeti lolote la serikali ambalo limetangaza kwamba kesi fulani zinapaswa kufanyiwa upelelezi ili kesi iweze kusikilizwa na haki iweze kutendeka” amesema
Anasema hata mawakili ambao wanaendesha kesi hizo lazima watangazwe na gazeti la serikali lakini uzoefu unaonesha kwamba mawakili wa serikali wanakwenda Mahakamani kuendesha kesi za uhujumu uchumi bila kupata uthibitisho wa uhalali wa kuendesha mashtaka hayo.

Wakili Madeleka ambaye amewahi kukaa Magerezani mawili la Segerea na Arusha kwa mwaka mmoja na mwezi mmoja akiwa na mke wake kutokana na kubambikizwa kosa la uhujumu uchumi
Anasema akiwa gerezani aligundua watu wengi waliojaa kwenye magereza hayo wanasota ndani kwa makosa ya aina hiyo.

“Nimekaa gerezani mawili tofauti la Segerea na Arusha kwa muda wa mwaka mmoja na miezi saba pamoja na mke wangu kwa kosa la uhujumu uchumi ambalo kimsingi nilibambikizwa kwa sababu ambazo nashindwa kuzielewa,
Tangu tumempata Rais mpya naona ameanza kuonesha anapenda haki naamini atakuwa msimamizi mzuri kupitia watendaji wake wanaomsaidia majukumu.”anasema.

Amesema anaongea mambo hayo licha ya kuyapitia akiwa gerezani lakini anauozefu mkubwa baada ya kudumu kwenye kitengo cha upelelezi kwa Jeshi la polisi nchini kwa miaka 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles