WAKENYA WASHIKA NAFASI YA JUU UTENDAJI KAZI UGHAIBUNI

0
817

 

NAIROBI, Kenya


WAHAMIAJI  kutoka nchini  hapa  wanaofanya kazi  nchini Marekani,  wameorodheshwa katika nafasi ya tatu kati ya raia wa kigeni wanaofanya kazi kwa bidii zaidi nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu iliyotolewa juzi na  Taasisi ya Bloombeerg ya nchini Marekani, wafanyakazi  raia wa wa Kenya walipata alama 73.4 kuchukua nafasi ya tatu miongoni mwa wafanyakazi wenye ujuzi zaidi na bidii nchini Marekani.

Utafiti huo unawaweka raia wa Ghana katika nafasi ya kwanza na wa Bulgaria kwenye nafasi ya pili wakiwa na asilimia 75.2 na 74.2.

Nchi nyingine  za Afrika zinazotajwa katika orodha ya 10  bora ni Ethiopia nafasi ya nne, Misri nafasi ya tano, Nigeria nafasi ya nane na Liberia nafasi ya tisa.

Hii imefanya waafrika kwa jumla kuwa wahamiaji wenye mazao ya juu zaidi nchini Marekani mbele ya raia  kutoka Mexico na Amerika ya kati wanaochukua asilimia 70 ya raia wa kigeni wanaoishi Marekani.

“Ikiwa tunataka wafanyakazi wenye ujuzi wa juu na wenye bidii wanozungumza lugha ya Kingereza sehemu bora ya kuelekea ni Afrika,”alisema Mwandishi wa Habari wa Taasisi hiyo ya Bloombeerg, Justin Fox, ambaye aliandika ripoti hiyo.

Ripoti hiyo iliyotokana na utafiti wa mwaka 2016 pia ilisema kuwa nchi hii ni kati ya za Afrika

Kulingana na ripoti hiyo Kenya, Ghana, Nigeria na Nepal zina raia wengi wanaosomea elimu ya juu nchini Marekani baada ya Saudi Arabia.

Ripoti hiyo ilisema kuwa idadi ya wakenya wanaoshi kihalali na kufanya kazi nchini Marekani kuwa 120,000

Ripoti hiyo inakuja miezi mitatatu baada ya utafiti wa Benki Kuu ya hapa  kuonyesha kuwa Wakenya wanaoishi na kufanya kazi nchi za nje walituma dola milioni 645 kati ya mwezi Januari na Machi mwaka 2018.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here