Rais Dkt John Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili kufuatia mualiko wa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta.
Ziara hiyo yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kibiashara baina ya Kenya na Tanzania imeleta mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa kwa Wakenya.
Katika mjadala huo, wengi wameonyesha hisia zao hasa katika kuchukizwa na tatizo la rushwa nchini mwao hivyo kuomba msaada kwa Rais Maguli kiwasaidia namna ya kuondokana nalo.
Wamekuwa wakitoa mawazo yao na kuomba msaada wa kumpa Rais wao mbinu za kupambana na rushwa huku wakitumia neno #MagufuliInKenya.
Wengi wao wanaomba kabla hajaondoka nchini humo amuachie Rais Uhuru Kenyatta muongozo yakinifu wa namna ya kupambana na rushwa.
Haya hapa ni baadhi ya maoni ambayo waKenya wameyatoa:
@musaomri ;Â #MagufuliInKenya can be consulted by @UKenyatta on how to handle corrupt officials in state offices #MinistryofHealthFacts.
@Gilbertich ; Welcome @MagufuliJP To our beloved country, please advice our beloved heads of state to stop corruption #MagufuliInKenya
@KiKimathi; KaribuKenya Magufuli. Hoping that these leaders will take notes on how to fight this corruption menace #MagufuliInKenya
@kaytrixx ; #MagufuliInKenya He should leave our gov’t with his marking scheme for fighting corruption.
@freddy_mckers ; The no nonsense president is in Kenya, this is great hope he will advice jubilee government on to deal with corruption #MagufuliInKenya
Je, Una maoni gani kuhusu waKenya kutaka wasaidiwe na Rais Dkt Magufuli katika kupambana na Rushwa.