24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAKENYA WAANDAMANA KUPINGA UFISADI

NAIROBI, KENYA

WANANCHI nchini Kenya wanafanya maandamano makubwa katika miji mikubwa ya nchi hiyo kulaani ufisadi wa mabilioni ya dola katika Serikali pamoja na kupinga kutokamatwa kwa baadhi ya washukiwa.

Mijadala juu ya kashfa za ufisadi imetawala mitandao mbalimbali ya kijamii huku vyombo vya habari vikizidi kufichua majina ya watu walionufaika kulipwa fedha pasipo kufanya kazi yoyote.

Kampeni kubwa inayoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter, Wakenya wanasema wamechoshwa na maofisa wa Serikali kuiba fedha zao na kuachiliwa huru.

Maandamano hayo yanafanyika baada ya kukamatwa na kushtakiwa kwa washukiwa 20 kati ya 50 waliokuwa wamekamatwa kutokana na sakata la ufujaji wa kiasi cha shilingi za Kenya bilioni 8 sawa na dola milioni 78 kutoka kwa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa (NYS) nchini Kenya kufikishwa mahakamani.

Miongoni mwa walioshtakiwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Vijana na Jinsia, Lilian Mbugua Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Richard Ndubai.

Aidha, mameneja wa kampuni ambazo zinadaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo walifikishwa kortini Milimani, jijini Nairobi. Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yanayohusiana na kutoweka kwa dola milioni 5 kati ya takribani dola milioni 80 zilizopotea katika shirika hilo la NYS.

Licha ya kukamatwa na kushtakiwa kwa baadhi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za umma, raia wanasema hawana imani kuwa wahusika watakabiliana na mkono wa sheria, kutokana na kwamba washukiwa katika sakata za ufisadi uliofichuliwa vipindi vilivyopita waliachiliwa.

Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekumbwa na sakata kadhaa katika siku za hivi karibuni katika kile kinachoonekana kushindwa kwa juhudi za kupambana na ufisadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles