25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wakenya kunywa maziwa, soda na vitafunio mazishi ya Moi

Nairobi, Kenya

WAOMBOLEZAJI katika mazishi ya Rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi wamehimizwa kuwahi mapema kwenye mazishi ili wapate maziwa na viburudisho vingine.

Serikali ya Kenya imesema itatoa viburudisho kwa watu 30,000 wa kwanza kufika katika mazishi  hayo yatakayofanyika leo.

Mratibu wa jimbo la Rift Valley,  George Natembeya amesema kuwa kutakuwa na viti, soda, maziwa na mikate pamoja na maji kwa watu 30,000 wa kwanza kufika kwenye mazishi na pia watakalishwa kwenye hema.

Natembeya amesema waombolezaji waliosalia watakaribishwa tu ndani ya eneo la makazi, lakini hawatapata mahala pa kukaa.

Amesema pia kwamba vitafunio vitatolewa kwa wale wa kwanza watakaohudhuria mazishi.

“Atakayefika kwanza ndiye atakayepewa wa kwanza “, alisema Matembeya huku akiwataka waombolezaji kufika mapema.

Aidha usafiri utatolewa kuanzia mji wa Nakuru hadi katika makazi ya Moi ya Kabarak yapata kilomita 20 (sawa na maili 12.4) kutoka Nakuru mjini.

Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa vigezo vya kauli hiyo ya Serikali ya kutolewa kwa viburudisho vya bure kwa waombolezaji.

Kupitia ukurasa wa Twitter Modal realism@MozDefinitely amesema serikali inaogopa sana kuwa idadi ya watu watakaojitokeza kwenye mazishi itakua ya chini, kwa hiyo imelazimika kuwahonga wakenya wasio na ajira kuhudhuria mazishi?.

@kamau_wanjohi anasema njaa na kiu ni kichocheo cha kutosha cha kuwavutia watu kuhudhuria mazishi.

Naye Kimathi @CounselKimathi ameandika Wakenya wanapaswa kuangaliwa kama wanajua wanachokitaka.

Tunachokihitaji sio mkate na soda ndogo…tunaweza kujinunulia hizi wakati wowote kwenye maduka. Tunataka kuona maendeleo” aliandika kupitia Twitter;

Ken Mapesa alishauri tofauti, ambapo alisema wangetoa maziwa badala ya soda wakati wa mazishi ili wakumbuke maziwa aliyoyatoa Moi wakati wa utawala wake kwa watoto wa shule yaliyojulikana kama Maziwa ya Nyayo:

Rais mstaafu Moi aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Jumanne wiki iliyopita na Wakenya mbalimbali wamekua wakipata fursa ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo aliyeliongoza taifa lao kwa muda wa miaka 27.

Mwili wa Hayati Moi utazikwa katika makazi yake ya Kabarak eneo la Nakuru siku ya Jumanne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles