29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Wakazi wa Bonyokwa washangilia kupata maji

Tunu Nassor, Dar es Salaam

Kwa mara ya kwanza wakazi wa kata ya Bonyokwa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo wameanza kupata huduma ya Majisafi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa kupeleka maji katani hapo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao wameshangilia kupata huduma hiyo kutokana na kutokuwa na kuikosa kwa miaka mingi.

Mmoja wa wakazi hao, Saumu Ally amesema kupatikana kwa huduma hiyo kutawasaidia kufanya shughuli zingine za maendeleo baada ya kuwa wanatumia muda mwingi kutafuta maji. 

“Tunashukuru sana sasa hata tukioga tutapendeza maana tumekuwa tukinywa maji ya visima ambayo tuliyanunua kwa bei kubwa,” amesema Saumu.

Naye Athanas  Masaka amesema ni historia  kwa Bonyokwa kushuhudia maji ya Bomba yakitoka katika eneo hilo.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam  (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema zaidi ya wateja 1,500 wameunganishiwa huduma hiyo.

“Mradi utawahudumia wakazi 30,00 wa kata hii ambapo tayari mabomba ya inchi 8,4,3, na 2 yamelazwa,” amesema Luhemeja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles