24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi mkoani Mwanza washauriwa kulinda makaburi ya Mv Bukoba

SHEILA KATIKULA, MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka wananchi mkoani hapo washirikiane na serikali ili kulinda makaburi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya meli ya Mv Bukoba mwaka 1996.

Amesema hayo Mei 21 mwaka huu kwenye kumbukizi za maadhimisho ya meli hiyo mkoani hapo, huku akisema ajali hiyo ni kama ajali nyingine.

“Tangu itokee ajali hiyo, imekuwa ni kielelezo cha kukumbushana katika umakini, bidii na kuendesha vyombo vya majini,” ameeleza.

Amesema tangu kutokea kwa ajali hiyo kuna sheria zimebadilika za usimamizi wa usafiri wa majini, nchi kavu na angani, lengo la serikali ni kuhakikisha taratibu zinafuatwa kwa umakini na kutoa elimu kwa wasafiri na waendeshaji wa vyombo hivyo.

“Sheria zimebadilika za usimamizi wa usafiri wa majini, angani na nchi kavu ndiyo maana serikali imeanzisha wakala Tasaki inayosimamia huduma za meli na usafirishaji ili kutoa huduma nzuri katika sekta hii kwa kukagua vyombo hivi na kuhakikisha taratibu na sheria za ubora zinafuatwa kwa kubeba abiria kwa kiwango kilicho wekwa na usimamizi mzuri,” amesema Mongella.

Mongella ameongeza kwamba serikali imewekeza kwenye chuo cha ubaharia Mwanza na Dar es Salam katika ukanda wa Afrika Mashariki ili kuongeza ufanisi katika usafiri huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles